Yanga dhidi ya Simba, leo ilikuwa bonge la mechi na limeisha kwa sare ya bao 1-1, Yanga wakianza kufunga kupitia Amissi Tambwe kabla ya Simba kusawazisha kupitia Shiza Kichuya. Cheki picha za action mambo yalivyokuwa.
pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 1 Oktoba 2016
LIVE KUTOKA TAIFA: YANGA 1 VS SIMBA 1 (FULL TIME)
MPIRA UMEKWISHAAAA
-Kona ya Yanga, Haji Mwinyi anaruka hapa na kupiga kichwa, nusura aipatie Yanga bao inakuwa gaoal kick
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Simba wanaendelea kushambulia, lakini Yanga hawajalala nao wanajibu mashambulizi
GOOOOOOOOOOOO Dk 87, Simba wanapata kona safi baada ya krosi ya Bukungu. Inachongwana Kichuya,
Dk 85 Juma Abdul krosi yake iipatie Yanga bao baada ya Tambwe kupiga kichwa safi kabisa
Dk 84, mpira mzuri kabisa wa Mwanjale, Simba wanaingia vizuri lakini mawasiliano ya Mo Ibrahim na Blagnon yanaonekana kutokuwa mazuri
Dk 83, Yanga wanaingia vizuri hatari kwenye lango la Simba, wapi wanaokpoa hapa
SUB Dk 81, Msuva anaingia kuchukua nafasi ya Juma Mahadhi
SUB Dk 79, Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Haruna Niyonzima.
KADI Dk 77, Barthez analambwa kadi ya njano baada ya kuchelewesha muda
SUB Dk 77, Simba wanamtoa Ajib na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim
Dk 76, Kazimoto anageuka na kupiga shuti kali kabisa hapa, lakini ni goal kick
Dk 74, Simba wanapata kona, inachongwa lakini Yanga wanaokoa kwa ulaini kabisa kupitia Dante hapa
Dk 71, Juuko anaachia mkwaju mkali kwelikweli, mpira unapita juu kidogo kwenye lango la Yanga, goal kick
KADI Dk 71, Twite analambwa kadi ya njano baada ya kumlamba ngwara Kazimoto
KADI Dk 69, Zimbwe Jr analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo
DK 67, Yanga wanapata kona hapa na inakwenda kuchongwa na Haji Mwinyi. Goal Kick, Haji alijaribu shuti lakini limepaa buuu
Dk 64, Tambwe anawachambua mabeki wa Simba na kutoa krosi safi hapa lakini Simba wanaokoa katikati hapa
SUB Dk 62, Simba wanawatoa Lufunga anaingia Juuko Murshid, pia wanamtoa Mavugo na nafasi yake anachukua Blagnon Frederic
Dk 60 sasa, Yanga wanaonekana kutulia zaidi na kucheza taratibu kabisa huku Simba wakionekana kuhaha na hawajatulia kabisa
Dk 58 sasa, timu bado zinashambuliana kwa zamu, Simba wanakuwa na tatizo la kupoteza pasi mara kwa mara
Dk 55 Kazi ipo, Lufunga na Tambwe hapa, Lufunga anampitia Tambwe, yuko chini anatibiwa hapa
Dk 53, Simba wanashambulia, Kichuya anaingia na kupiga shuti kali lakini kuuuubwaaa
Dk 51,, Tambwe yuko chini, inaonekana kama Lufunga alirusha mkono wake ukampata usoni
Dk 50, Zimbwe Jr anafanya kaosa hapa, Kaseke anaingia anapiga kwosri hapa lakini Angban anadaka vizuri
Dk 49, Bukungu anapiga shuti kali ule mpira wa faulo, unagonga mwamba na kurudi, Mavugo anapiga shuti lakini unaokolewa
DK 48, Kichuya anawachambua mabeki wa Yanga, wanamuangusha inakuwa faulo
SUB Dk 47 Yanga inamtoa Yondani na nafasi yake inachukuliwa na Andrew Vicent au Dante
Dk 46, Simba wanaanza kwa kasi, Mwinyi anaingia na kumuangusha Kichuya hapa-
MAPUMZIKO
-Ajibu anawalamba chenga mabeki wa Yanga na kuachia shuti kali lakini ni goal kick
-KADI Yondani analambwa kadi ya njano baada ya kuchelewesha mpira
Dk 45 Kipa Barthez yuko chini pale akitibiwa baada ya kugongana na Juma Abdul baada ya kugongana
Dk 45, Mavugo anaingia vizuri, anamtola Juma Abdul na kupiga shuti, BArthez anaokoa na kuwa kona.
Dk 44, Yanga wanashambulia tena shuti hapa la Mahadhi lakini linakuwa dhaifu
Dk 43, Mavugo anajaribu shuti lakini linatoka nje sentimeta chache
Dk 42, Tambwe yuko chini pale baada ya kuangushwa na mwamuzi anaonya pale
Dk 40, Kichuya anaingia vizuri kabisa anaachia shuti kali lakini halikulenga lango
Dk 37, Ngoma anawachambua mabeki wa Simba kama karanga hapa na kuachia shuti kali kabisa, lakini Angbani anadaka vizuri
Dk 30 hadi 35, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja hata hivyo Simba wanaonekana hawajatulia baada ya kulalamikia lile bao la Tambwe ambaye alishika na kulalamikiwa na wachezaji hao
Dk 29, mpira bado umesimama, mashabiki wa Simba wanang'oa viti, polisi wanapiga mabomu ya machozi
KADI Dk 28 Mwamuzi anamlamba kadi nyekundu nahodha wa Simba Jonas Mkude, haijajulikana kama alifanya nini
Dk 27, walinzi wanalazimika kuingia uwanjani kuwapoeza wachezaji wa Simba wakilalamika kama wanasusia baada ya Tambwe kufunga bao hilo wakisema alishika GOOOOOOOOOOOO Dk 26, Tambwe anaipatia Yanga bao safi baada ya kugeuka na mpira ukiwa mkononi mbele ya Lufunga na kufunga kirahisi kabisa
Dk 24, Mpira wa kurushwa, Ajibu anaunganidha shuti juujuu hapa lakini anashindwa kulenga lango na mashabiki wa Yanga wanazomeee buuuuuu
Dk 23, Kichuya anaangushwa hapa, mwamuzi anasema faulo lakini yeye analalmika huku upande mwingine Bossou naye akiwa analalamika kwamba amepigwa kiwiko
Dk 22, Ajibu anajaribu kuwachambua mabeki wa Yanga, anaanguka lakini mwamuzi anamwambia amka twende kazini baba
Dk 20, Simba wanagomngeana vizuri zaidi lakini wanakuwa si wazuri katika kumalizia
Dk 16, Yanga wanaonekana kutulia zaidi na kucheza soka safi zaidi huku Simba wakihaha kuwakapa
Dk 14, Krosi nzuri ya Juma Abdul, Kamusoko anapiga kichwa kinatoka sentimeta chache nje juu ya lango la Simba
Dk 11, Mavugo anawekwa chini na Yondani, anatibiwa na kutolewa nje. Mpira unaendelea
Dk 9, mpira wa faulo wa Mavugo, unababatiza ukuta wa mabeki wa Yanga na kuokolewa
Dk 7, Zimbwe anatelekeza lakini anauwahi mpira na kuutoa, inakuwa kona,inachongwa
hatari hapaa, shuti la Tambwe linatoka sentimeta chache kabisa
Dk 6, Kichuya anatoa pasi nzuri kwa Ajib, anageuka na kupiga, mpira unaingia langoni. Lakini mwamuzi Saanya anasema ilikuwa offside tayari
DK 3, Kazimoto anaangushwa wakati akienda kufunga, mwamuzi anasema faulo, anaipiga Ajibu lakini juuuuu
Dk 1, mechi imeanza taratibu na Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Simba.
LIVE KUTOKA TAIFA: GOLI LA MKONO LA TAMBWE LAZUA GUMZO YANGA 1 VS SIMBA 0 (KIPINDI CHA KWANZA)
Dk 45, Mavugo anaingia vizuri, anamtola Juma Abdul na kupiga shuti, BArthez anaokoa na kuwa kona

VIKOSI VYA SIMBA VS YANGA LEO Kikosi cha SimbaVicent AngbanBesala BokunguMohamed Hussein ShabalalaNovart LufungaMethod MwanjaliJonas MkudeShiza KichuyaMzamiru YassinLaudit MavugoIbrahim AjibuMwinyi KazimotoSubPeter Manyika Abdi BandaJuuko MurshidSaid NdemlaMohamed IbrahimFredrick BlagnonJamal Mnyate Kikosi cha Yanga1. Ali Mustafa2. Juma Abdul3. Haji Mwinyi4. Kelvin Yondani5. Vicent Bossou6. Mbuyu Twite7. Juma Mahadhi8. Thabani Kamusoko9. Amisi Tambwe10. Donald Ngoma11. Deusi KasekeAkiba- Deogratius Munishi- Hassani Kessy- Oscar Joshua- Nadir Haroub- Saimoni Msuva- Haruna Niyonzima- Obrey Chirwa- Yusufu Mhilu
Je wajua Upinzani wa Simba na Yanga ulianzia hapa…
Ipo itikadi hata wengine huamini kwamba, utambulisho wa mtanzania ni alama ya chanjo ya mwili maarufu kama ‘ndui’ ambayo inapatikana kwenye bega mojawapo la mwilini mwa binadamu. Lakini ukizungumza habari ya soka la Tanzania, lazima uguse uwepo wa vilabu viwili vya Simba na Yanga ambavyo vimetokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa vijana katika shughuli mbalimbali itikadi pia ikichangia kuanzishwa kwa timu hizi. Yanga ndiyo kongwe kiumri ikiwa imeanzishwa rasmi mwaka 1935 Simba ikifuata mwaka mmoja baadaye 1936 ikiitwa Sunderland jina ambalo lilitokana na timu mojawapo ya ligi ya England wakati Yanga ilikuwa ikifahamika kwa jina la Young Africans SC ambalo ni chimbuko la jina la kimarekani. Baadaye viongozi wa serikali walivitaka vilabu hivi kubadilisha majina yao na kutumia majina halisi ya kiafrika na kuondoka kwenye majina ya kigeni, hapo ndipo tukapata Simba na Yanga. Vilabu hivi vimejenga upinzani mkubwa katika soka la Tanzania tangu mwaka 1936 wakati huo ikichezwa ligi ya mkoa wa Dar es Salaam (Dar es Salaam League) hadi mwaka 1965 ilipoundwa ligi ya taifa lakini hadi leo vimekuwa vikiumiza vichwa vya mashabiki lukuki wa soka ndani na nje ya nchi kutaka kujua nani ataibuka na ushindi pale vidume hivi viwili vinapokutana. Kwa mujibu ya mazungumzo ya wazee wa zamani, wanasema upinzani wao ulitokana na vyanzo vya kibaguzi. “Yanga na Simba sio kuna upinzani, kuna uadui. Uadui na upinzani wetu umeanzia pale timu ilipogawanyika kutokana na ubaguzi, kundi moja likiwa la waarabu jingine likiwa la wamatumbi, wandengereko na wazaramo”. Matokeo yoyote ya timu hizi hugusa mashabiki kwa hisia tofauti, wengine huwa na shangwe kubwa wakati upande mwingine wakilia na kupoteza fahamu. Oktoba 1 timu hizi zinakutana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, wanakutana kwa mara ya kwanza kwenye msimu wa 2016-2017 huku Simba wakiingia uwanjani wakiwa na machungu ya kupoteza michezo miwili mfululizo katika msimu uliopita wakikumbuka machungu ya September 26 mwaka uliopita sambamba na February 20 mwaka huu. Takwimu zinaniambia timu hizi zimekutana mara 92 kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara, Yanga ikiongoza kwa kushinda mechi 35 na ikiwa imefunga magoli 101 wakati Simba mechi 25 na kufunga magoli 88 huku sare zikiwa 32. Mbali ya rekodi hiyo, tukiwatazama makocha wote wawili wamekuwa na historia ya tofauti. M-cameroon Joseph Omog ni kocha mpya wa Simba kwa sasa akiwa na michezo sita tu, ameshinda mechi 5 na kutoka sare mchezo mmoja. Kumbuka kocha huyu amerejea kwa mara ya pili, awali alikuja kuifundisha Azam FC ambapo aliipa ubingwa wa kwanza wa ligi. Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi yeye amesimama Yanga akiwa na rekodi lukuki ikiwemo kutwaa mataji matatu, mawili ya ligi na moja la FA lakini pia kuwafuta Yanga tongotongo za macho zilizodumu kwa miaka 18 tangu mwaka 1998 walipofuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika hadi walipofuzu tena mwaka huu robo fainali ya kombe la shirikisho. Katika rekodi nyingine, tangu Pluijm alipoifunga Simba February 20 mwaka huu, amecheza mechi 16 akishinda mechi 11 sare mechi nne na kupoteza mchezo mmoja wakati katika mechi 16 Simba ilishinda mechi 10 sare tatu na ikapoteza mechi tatu. Takwimu zinaendelea kuonesha, katika mechi hizo 16 Yanga imefunga magoli 34 Simba ikifunga magoli 22 wakati Yanga ikiruhusu wavu wake kuguswa mara 12 Simba imeruhusu wavu wake kuguswa mara 6 ikiwa ni nusu ya magoli waliyofungwa Yanga ndani ya mechi 16. Mechi 7 za Yanga zilimalizika kwa ‘clean sheet’ yaani bila kuruhusu goli wakati Simba wakimaliza bila kuruhusu bao kwenye mechi 11. Ndani ya mechi 16, Yanga ilikusanya pointi 37 huku Simba ikitwaa pointi 33, Yanga ikapoteza pointi 11 huku Simba wakipoteza jumla ya pointi 15 katika michezo 16. Kilichobaki ni macho na masikio ya wapenzi wa vilabu hivi kujua nini watafanya watani hawa wa jadi pale katika uwanja wa taifa chini ya usimamizi wa Martin Saanya. Je, Yanga wataendeleza ubabe au Simba watajibu mapigo katika msimu huu?
Apa baba apa mwana apatoshi sikia hii Kisa cha Haji Manara kuzaliwa familia ya Yanga lakini akaishabikia Simba
Kama ulikuwa hujui basi nakupa hii, afisa habari wa klabu ya Simba SC Haji Manara amezaliwa kwenye familia ya mchezaji wa Yanga, Sunday Manara ambaye ni baba mzazi wa Haji Manara alikuwa ni mchezaji wa Yanga na sasa amebaki kuwa mwanachama wa klabu hiyo.
Cha ajabu na kinachoshangaza ni kwamba, licha ya Haji Manara kuwa ni mtoto wa mchezaji wa Yanga bado yeye mapenzi yake yalikuwa pale mtaa wa Msimbazi kwa mnyama Simba na akakua akiwa anaipenda Simba.
Kutana na Sunday Manara baba mzazi wa Haji Manara kwasasa akiwa ni shabiki wa Yanga, mtoto wake Haji Manara ni mwanachama na msemaji wa klabu ya Simba, Sunday Manara amemuelezea mwanae kwa nini amekuwa shabiki wa Simba.
“Babu yake Haji mzaa mama alikuwa mwenyekiti wa Simba na tulikuwa karibu sana na yule mzee, haya ni mapenzi ya mchezo bado sisi wote ni wamoja tofauti za Yanga na Simba zibaki kwenye mapenzi ya mchezo wa mpira lakini iwe dhamira imejengeka na wote tunakusudia kujenga kitu kimoja, mpira wa Tanzania uende juu”, alisema Sunday Manara ambaye ni baba mzazi wa Haji Manara.
“Bahati mbaya fikra za watu wanafikiri Yanga na Simba ni uadui kwasababu hawaelewi, huu sio uadui. Mimi ninarafiki zangu wengi ni wapenzi wa Simba. Haji kwenda kwake Simba hakufanyi asiwe mwanangu, mimi ni mpenzi wa Yanga si mpenzi wa Simba”.
“Nina mwanangu mwingine jina lake Manara ni shabiki wa Simba, mtoto mdogo wa Haji ni shabiki wa Yanga, walishampeleka hadi klabu ya Simba wakampa soda na kilakitu wakamuuliza anapenda timu gani akasema Yanga lakini hakuna uhasama wala chuki”.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)