LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: SIMBA 0 VS AZAM FC 0 Dk 36 sasa, bado si mechi ya kuvutia sana kama ambavyo ilikuwa imetarajiwa
KADI Dk 33, Erasto Nyoni analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Pastory Athanas, hii ni kadi ya kwanza ya njano ya mchezo huu
Dk 30, hakuna timu iliyogusa nyavu na mpira unaendelea kuchezwa katikati zaidi ya uwanja na tahadhari kubwa yenye uoga ikiendelea kuchukua nafasi
Dk 23, Yakubu anautoa mpira nje na kuwa kona ya kwanza ya mchezo ambao wanaipata Simba. Inachongwa hapa Azam FC wanaokoa
DK 20 sasa, kila timu iko makini sana. Maana walinzi ni wanne kwa kila upande na kila timu inaposhambuliwa inakuwa na walinzi zaidi ya watano
Dk 15, Mahundi anapoteza nafasi nzuri ya kwanza baada ya kuupata mpira kwenye boksi la Simba mabeki wakiwa wamezubaa, anapiga shuti la chini, mpira unampita Agyei na kuwa goal kick
Dk 13, Bocco anajaribu hapa katika lango la Simba lakini Agyei anakuwa makini na kuudaka mpira huo
Dk 9, Bukungu anaachia shuti kali lakini linatoka nje. Kinachoonekana timu hizi kila mmoja imejaza watu wengi zaidi nyuma, hivyo kufanya kusiwe na ladha ya juu ya ushambulizi
Dk 6 sasa, hakuna shambulizi hata moja kali. Zimbwe wa Simba anatolewa nje baada ya kugongana na Mhundi, anapatiwa matibabu
Dk 2, Azam FC wanakuwa wa kwanza kufika lango la Simba lakini shuti la Mahundi, linadakwa kwa ulaini na kipa Agyei
Dk 1, mechi imeanza taratibu kabisa huku kila timu ikionekana inataka kuusoma mpira au mbinu za mwenzake kabla ya kuzipambanua zake
HEAD TO HEAD SIMBA VS AZAM FC
Kutana mara 17
Simba shinda mara 8
Azam Mara 4
Sare 5
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni