LIVE KUTOKA AMAAN, ZANZIBAR: YANGA 0 VS SIMBA 0 (KIPINDI CHA PILI) Dk 47 krosi nzuri ya Mwinyi lakini Mwanjale anauwahi, kona. Inachongwa na Niyonzima , wanaokoa
Dk 46, Yanga wanacheza vizuri, lakini Tambwe anashindwa kupiga krosi kutokana na kasi ya mpira
Dk 45, Kipindi cha pili kimeanza na inaonekana suala la hofu kwa wachezaji bado limejaa
MAPUMZIKO
KADI Dk 45, Mwamuzi anatoa kadi ya njano kwa Abdi Banda kumuangusha Kaseke, kadi ya njano kwa Juma Abdul
Dk 43, hatariiiii, Msuva anapoteza mpira, Mo Ibrahim anaachia fataki, Dida anaugusa na kutgonga mwamba, unamkuta Luizio anaachia shuti, goal kick
Dk 40, Banda anaachia fataki lakini mpira unawagonga mabeki wa Yanga, wanaokoa
KADI Dk 39, Mwingi analambwa kadi ya njano kwa kumrukia Mo Ibra
Dk 37, Msuva anamtoka Zimbwe kwa mara ya kwanza, anaingia vizuri na kujaribu kupiga lakini mpira anaukosa na Bukungu anauokoa kabla haujavuka lango
Dk 34, Dida anafanya kosa hapa, nusura Bukungu lakini anaitahi kuuwahi
Dk 34 mechi bado inaonekana kuwa ngumu, kila upande una mashambulizi lakini si uhakika
Dk 28, Yanga inapata kona baada ya Simba kuukoa mpira wa faulo wa Mwinyi, inachongwa lakini kipa anafanyiwa madhambi
Dk 21 sasa, mambo bado, mashambulizi si mengi. Simba hasa Banda wanapaswa kuwa makini na kupunguza mipira isiyokuwa na maana karinu lango lao
Dk 18, mkwaju mkali wa Mwinyi wa faulo, unatoka kidogo nje ya lango la Simba
Dk 16, Mo Ibrahim, anaachia shuti kali katikati ya msimu wa mabeki wa Yanga, Dida anadaka vizuri kabisa
Dk 15, Yanga wanapoteza nafasi, Msuva anapiga shuti lakini Banda anakaa chini na kuzuia. Ilikuwa nafasi nzuri kwa Yanga
Dk 10 sasa, kila upande unaonekana kuwa makini sana kwa sababu hakuna mashambulizi mengi kwenye milango
Dk 8, Banda anapiga kichwa mpira unamkuta Niyonzima, anaingia vizuri na kuachia shuti kali hapa, Agyei anadaka vizuri kabisa
Dk 7, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja ingawa Simba ndiyo wanaonekana kutawala zaidi katikati ya uwanja
Dk 3Yanga wanaanza kuwa wa kwanza kuingia kwenye lango la Simba lakini Mwanjale anakuwa makini
Dk 1Mechi imeanza kwa kasi kubwa huku ikionekana kila timu imepania kupata bao la mapema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni