pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 3 Desemba 2016
USAIN BOLT, ALMAZ WANARIADHA BORA WA MWAKA DUNIANI Mjamaica Usain Bolt na Mhabeshi Almaz Ayana wakiwa wameshikilia tuzo zao za Wanariadha Bora wa kiume na wa kike wa Mwaka kutoka Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF) baada ya kukabidhiwa jana mjini Monaco, Ufaransa. Usain Bolt alitwaa Medali yake ya tisa ya Dhahabu ya Olimpiki baada ya kutwaa tena mjini Rio mwaka huu na sasa kijana huyo wa umri wa miaka 30 atastaafu mwakani baada ya michuano ya Dunia, akikimbia mbio za mita 100 na relay ya 4x100 katika msimu wake wa mwisho.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni