Jumamosi, 3 Desemba 2016

Ronaldo na Mourinho wanahusishwa na kasha ya nzito ya ukwepaji kodi. Kama ni kweli kwa muda wote huo wamefanikiwa kuficha wizi wanaofanya kwenye swala zima la kodi basi watakua walikua wanatumia mbinu kali sana. Gazeti moja la uchunguzi linaitwa Der Spiegel nchini Ujerumani wametoa ripoti na kusema kwamba wateja wawili wa wakala Jorge Mendes wamekwepa kodi yenye thamani ya kiasi cha Euro milioi 150. Gazeti hilo limetoa ripoti kwamba walifanukiwa kufanya hivyo kwa udanganyifu ambao ulisaidiwa kwa kuficha pesa kwenye benki zilizopo nchini Switzerland au British Virgin Islands. Ripoti hiyo ambayo imetoka sehemu ya kwanza tu imepewa jinala Football Leakes inaripiti kwamba mchezeshaji mkuu wa mchezo huu ni Jorge Mendez na kampuni yake. Kampuni ya Gestifute inayomilikiwa na bwana Mendes hawajakaa kimya kuhusu wateja wao kupewa kasha hii. Sehemu ya tamko lililotolewa linasema kamba hakuna kati ya wateja wao hao wawili wamefanya mikotaba yoyote iliyohusisha ukwepaji wa kodi. Wameongeza kwamba kila kitu kilifata sheria na taratibu za kodi kwenye nchi za England na Spain. Gazeti hilo limesema hii ni sehemu ya kwanza ya ripoti yao. Wanakuja na sehemu ya pilku ya ripoti hii ambayo itaweka wazi ushahidi jinsi Mendes alivyochezesha ukwepaji huu wa kodi kwa wateja wake wanahusika na kias kikubwa cha pesa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni