Jumatano, 2 Novemba 2016

LIVE KUTOKA SOKOINE MBEYA: MBEYA CITY 1 VS 0 YANGA

Dk 22, City wanagongeana vizuri tena, Mahundi hatari huyu, anaachia shuti kaliii, hatari kabisa unatoka sentimeta chache kabisa kwenye lando la Yanga Dk 21, Yanga wanagongenaa vizuri hapa, mpira unamfikia Msuva anaachia fataki....wapiii Dk 19, kipa wa Mbeya City anaokoa mpira hatari wa Donald Dombo Ngoma SUB Dk 19 upande wa Mbeya City, Hemed Mlutabozwa anatoka baada ya kuumia, anaingia Hemed Ramadhani. Dk 15, Mbeya City nao wanapata kona baada ya krosi ya Maundi kuokolewa na kutoka. Mwasapili ndiye anachonga hapaa, Yanga wanaokoa Dk 14, Msuva anamtoka Mwasapili, krosi safi kabisa lakini City wanaokoa na kuwa kona ya pili Dk 13, Msuva anaingia vizuri na kupiga krosi, inaokolewa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina matunda Dk 11 sasa, bado Yanga wanaonekana hawajatulia wala kufanya shambulizi kali linaloweza kuwapa City presha GOOOOOOO Dk 6, Hassan Mwasapili anapiga mpira unaojaa moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa Dida Munishi Dk 1, kila timu imeanza taratibu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini hakuna inayocheza kwa papara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni