Alhamisi, 1 Septemba 2016

Ni Ajib Yanga, hakuna namna KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm humwambii kitu kuhusu beki wake, Andrew Vicent ‘Dante’. Anamsifia Dante kwa jinsi anavyopiga vichwa licha ya ufupi wake. Lakini beki huyo amewaambia Yanga kwamba hata wakikutana na Simba leo mchezaji anayeweza kuwasumbua ni Ibrahim Ajib. Wala si Laudit Mavugo wala Muivory Coast Fredrick Blagnon. Dante amewaaminisha Yanga kwamba hao wanakabika kirahiiisi kinoma wala hana mzuka nao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni