pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 1 Septemba 2016
Mzungu na Kessy mbona mzuka tu KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm amemtazama beki wake wa kulia Hassan Kessy anavyocheza na kusema anazidisha chumvi hivyo ipo haja ya kumuita na kumtuliza mzuka alionao. Alisema Kessy ni mchezaji mwenye umri mdogo na wachezaji wa aina yake huwa wanataka kufanya kila kitu uwanjani na kuzidisha wanayofundishwa lakini atamtuliza ili akae vizuri. Kessy amejiunga Yanga msimu huu na katika mechi ya ufunguzi na African Lyon alionekana kukaba vizuri lakini alipopanda alitaka kupiga krosi, pasi na chenga kwa pamoja.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni