Jumapili, 18 Desemba 2016

Shime aukubali mziki mnene wa Yanga Huwezi kufunga kama unapoteza nafasi – Shime. Akisimama kwa mara ya kwanza kama kocha wa JKT Ruvu, Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ amewapongeza wachezaji wake pamoja na Yanga kwa kupata ushindi. Shime amesema huwezi kufunga kama unapoteza nafasi unazozipata, lakini kocha huyo aliyefanya vizuri na kikosi cha Serengeti Boys amesema anaamini timu yake itafanya vizuri kwenye mechi zijazo baada ya kufanya marekebisho kwa makosa aliyoyaona wakati wa mchezo dhidi ya Yanga. “Kutokufunga wakati mwingine ni kupoteza nafasi ambazo umezipata huwezi kuona kwamba Yanga wametufunga kwa uhodari mkubwa lakini ni kwa makosa binafsi ya mchezaji mmojammoja ndiyo yamepelekea Yanga kupata matokeo yale.” “Kama mwalimu nawapongeza vijana wangu naamini watafanya vizuri katika mchezo unaofata.” “Lakini pia niwapongeze wapinzani wetu kwa kupata ushindi, mechi ilikuwa nzuri lakini magoli tuliyofungwa hayaendani na uzito wa mechi tuliyocheza.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni