Jumapili, 18 Desemba 2016

Soka halihitaji maneno-maneno, kazi uwanjani – Niyonzima Kiungo mshambuliaji wa Yanga Haura Niyonzima ‘Fabregas’ amesema mchezo wa soka hauhitaji maneno mengi badala yake kazi ionekane uwanjani. Niyonzima alicheza katika kiwango cha juu kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa magoli 3-0 matokeo yaliyoiweka Yanga katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa VPL wakisubiri matokeo ya Ndanda FC vs Simba kuamua kama Yanga itaendelea kukaa katika nafasi ya kwanza au itashushwa. “Mchezo wa mpira hutakiwi kuzungumza mengi, sisi tuko vizuri lakini kila mechi inakuwa na mambo yake. Mechi hii imeisha inabaki kuwa historia, naamini kwa ushirikiano wa wachezaji wote na mwalimu tutafanya vizuri,” anasema Niyonzima ambaye alicheza dakika 90 dhidi ya JKT Ruvu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni