Jumatano, 2 Novemba 2016

Simba watakaa tu, hakuna namna – Kocha Stand United

Kocha wa Stand United Athuman Bilal ambaye ameachiwa timu na mfaransa Patrick Liewig, ameshakiongoza kikosi hicho katika mechi 5 akishinda mechi moja, sare tatu na kupoteza mechi moja. Leo atakuwa kwenye mtihani mwingine katika kibarua chake atakaposimamia bechi la ufundi kuiongoza Stand United kuikabili Simba SC kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Bilal amesema hana hofu na Simba kwasababu tarari anarekodi ya kuwafunga na anawamudu vizuri huku akisisitiza kuwa, anajua namnaya kucheza na timu kubwa. Tunaingia kwa ajili ya kuifunga Simba “Tunaingia kwa ajili ya kushinda, Simba ni mpinzani wetu kwasababu hadi sasahivi bado hajafungwa sisi tumepoteza mchezo mmoja, tukiwafunga tunaendelea kubaki kwenye nafasi nzuri na lengo letu ni kubaki katika nafasi za juu, kwahiyo Simba lazima afungwe.” Safu bora ya ulinzi Stand ni miongoni mwa timu ambazo zimeruhu magoli machache ya kufungwa, hadi sasa wamefungwa magoli 9 baada ya kucheza mechi 13. Kocha wa Stand amesema anajivunia kuwa na safu bora ya ulinzi iliyokaa kwa muda mrefu. “Namshukuru Mungu nina safu bora ya ulinzi inayoundwa na vijana waliocheza pamoja kwa muda mrefu, vijana ambao nilikuwa nao tangu Toto Africans sasa hivi tupo pamoja Stand. Najisifia kwa hilo, nawaamini vijana wangu watafanya kazi nzuri dhidi ya Simba.” Simba ni mpinzani wetu Hadi sasahivi Simba bado haijapoteza mechi yeyote, wamecheza mechi mbili nje ya Dar na wameshinda zote lakini Bilal anasema Simba anauwezo nayo na wasitarajie mteremko kutoka kwa Stand United. “Mwaka huu tumejipanga kiupinzani, Simba ninauwezo nayo nasubiri kuwastaajabisha watanzania. Sijaona ubora wa Simba wala ugumu wake uko wapi kwasababu wachezaji wengi ni walewale wa nchi hii wameongezeka wachache ambao walikuwa Mtibwa tayari tulisha kutana nao hawatakuwa wapya.” Simba isitarajie goli la mapema Kocha huyo wa Stand amesema anajua kuwa kwenye mechi nyingi ambazo Simba wameshinda walipata goli la mapema ndani ya dakika 45 za kwanza, kwa upande wake amejiandaa kwa hilo na amesisitiza atafanya matukio muhimu kwenye dakika muhimu ili kuzuia mipango ya Simba. “Najua jinsi ya kucheza na timu kubwa, udhaifu wao uko wapi na wanataka nini katika dakika gani. Najua dakika ya ngapi nifanye nini, ntafanya matukio machache tu ya muhimu.” Bilal anavaa viatu vya Liewig Baada ya kuwafunga Yanga akiwa kama kocha msadizi chini ya Patrick Liewig, Bilal amesema baada ya kuondoka kwa mfaransa Liewig anataka kuonesha uwezo wake kwa kuifunga Simba kwasababu haitakuwa mara yake ya kwanza kuwafunga wakali hao wa Msimbazi. “Sio maa ya kwanza kuifunga Simba, nina misimu kama miwili hivi nawafunga. Nikiwa Toto niliwahi kuwafunga na nikiwa hapa Stand nimeshawafunga nikiwa kama kocha mkuu.” “Patrick ameondoka nimeifunga Azam ambayo ni timu kubwa.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni