pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 1 Novemba 2016
Chama cha mpira wa miguu cha Uingereza FA leo kimemshtaki kocha Jose Mourinho kwa utovu wa nidhamu alioonesha katika mechi ya Man United dhidi ya Burnley jumamosi ya wiki jana, Oktoba 29,2016. Imeripotiwa kuwa kipindi cha mapumziko Kocha huyo alitumia maneno mabaya kwa mwamuzi Mark Clattenburg,na kipindi cha pili akapelekwa jukwaani kwa mashabiki kutokana na kosa hilo. Jose aligeuka mbogo kwa mwamuzi huyo akidai kwa nini timu yake haikupewa penati pale Matteo Darmian alipochezewa vibaya na Jon Flanagan katika eneo la hatari. FA imemtaka Jose kujibu shtaka hilo kabla ya siku ya ijumaa ya juma hili.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni