Jumatatu, 10 Oktoba 2016

Pogba awnyamazisha wanao chonga dhidi yake na kumtaka kocho wa tim ya taifa ya Ufaransa kumpiga chini Goli lake la mita 30 lilivyoipa ushindi Ufaransa dhidi ya Uholanzi

Tayari yalishaanza maneno kwa kocha wa Ufaransa Didier Deschamps kwamba ampige chini kiungo wa Manchester United Paul Pogba kwenye kikosi cha Ufaransa kilichocheza dhidi ya Uholanzi. Nyota huyo mwenye miaka 23 amelipa fadhila za kuaminiwa na kocha wake baada ya kufunga goli pekee kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 dhidi ya Uholanzi Akiwa umbali wa zaidi ya mita 30 kutoka golini, Paul Pogba aliachia shuti kali ambalo lilimshinda golikipa wa Everton Maarten Stekelenburg licha ya kujaribu kupangua shuti hilo. Golikipa huyo mdachi alipambana kadri alivyoweza ili kuzuia shuti la Pogba lakini hakuweza kufanya kile ambacho alitarajia kukifanya na hatimaye kuzishuhudia nyavu zake zikicheza. Sasa huenda mashabiki wa Manchester United wakawa na matumaini mapya ya kumuona Pagba akifunga magoli mengine kama hayo akiwa kwenye klabu yake ya Old Trafford.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni