Jumanne, 11 Oktoba 2016

Je wajua Siri ya kiwango cha CR7 kwa sasa iko apa...

Na Victor Mengi Huwezi ukawa unampenda mchezaji na hujui kwanini unampenda mchezaji huyo, mimi ni mpenzi sana wa mchezaji Criastiano Ronaldo. Ninasababu mia kwanini ninampenda mchezaji huyu, Cristiano Ronaldo ni mchezaji anaeamini kwamba “hard work can beat talent” Cristiano Ronaldo ni mchezaji mwenye kiu ya mafanikio kuanzia maisha ya soka na maisha yasiyo ya soka. Kwake hakuna kufeli….. Cristiano Ronaldo si mtu wa starehe japo kuwa maisha yake binafsi ni mtu wa wasichana sana (hakuna anaethibitisha hili) wote tunasoma majarida mbali mbali ukiangalia documentary yake ya maisha yake kuna sehemu anasema “i might be wealthy but no one knows the hard work and sacrifices we make.” Kwa haya yote tutafikia kuzungumza form yake ya sasa tangu Euro mpaka hapa alipo akiwa hafanyi poa sana kwenye La Liga. Nikasoma nakala katika mitandao tofauti kama vile goal.com, shaffihdauda, skysports wote wamekuwa wakitabiri anguko lake. Mimi nimeona tofauti sana, Cristiano alikuwa na injury kabla hajaenda Euro akiwa katika ligi aliumia nakumbuka ilikuwa mechi ya La Liga vs Vilareal kama sikosei aliumizwa goti, CR 7 akaenda Champions League akijisukuma kibishi hadi wanachukua UEFA, akaenda vivyo hivyo hadi fainali alipogongwa sehemu ileile. Ni kwanini anadorora? Je ni kwa kuisha kiwango? Hapana CR 7 anajiona muhimu na ni muhimu katika timu zake zote. Zidane ameshindwa kumuweka bench CR 7 kwakuwa hayupo fit hapa ndipo utakapoona Fergie na Wenger ni zaidi ya makocha hawana tabia ya kulazimisha mchezaji asiye na match fitnes. CR 7 hajawa 100% fit katika hii miezi kadhaa iliyopita lakini makocha wake hawana namna inabidi achezeshwe…. Hivyo kinachomzingua CR 7 ni kukosa mtu wa kumkemea au wakumwambia sikuchezeshi huna match fitness kwasababu yeye anaona anafanya bidii lakini anajiumiza… So anguko la ubora wa CR 7 siyo majeruhi yake ila ni la makocha na wasimamizi wake katika timu zake zote mbili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni