Jumanne, 31 Januari 2017

BAADA YEYE NA KLOPP "KUSHINDWANA", SAKHO SASA ANUKIA CRYSTAL PALACE Klabu ya Crystal Palace imeonyesha nia ya kumpata beki Mamadou Sakho. Liverpool intake kulipwa pauni milioni 20 ili kumuachia beki huyo raia wa Ufaransa. Sakho na Kocha Jurgen Kloop aria wa Ujerumani wanaonekana kutoelewana kabisa. Wakati dirisha la usajili linakwenda ukingoni , inaonekana juhudi zinafanyika.

BAADA YA SIMBA KUITOLEA NJE, MAMELODI SASA KUIVAA AZAM ALHAMISI Baada ya kikosi cha Simba kutoa nje kucheza na Mamelodi, ssa timu hiyo itashuka dimbani Alhamisi, kuivaa Azam FC. Taarifa zinasema, Mamelodi wataendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi dhidi ya Azam FC hiyo Alhamisi, mechi inayotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Awali, Mabingwa hao wa Afrika walitakiwa kucheza kesho dhidi ya Simba, lakini klabu hiyo imeona ina majukumu ya maandalizi dhidi ya Majimaji mjini Songea, wikiendi hii. Lakini pia kumekuwa na taarifa kwamba waandaaji wa mechi hiyo hawakuwa na maandalizi mazuri kati yao na uongozi wa Simba kuhusiana na mechi hiyo. Hata hivyo, mmoja wa waandaaji amesema, Simba walikuwa na taarifa za kutosha lakini wamegeuka huenda inatokana na wao kupoteza mechi dhidi ya Azam FC Jumamosi na Yanga ikaishinda Mwadui FC na kukwea kileleni.

Jumatatu, 30 Januari 2017

SIMU INAWEZA KUMTIA PAUL POGBA MATATANI, USHAHIDI HUU HAPA…Kiungo wa bei kubwa wa Manchester United, Paul Pogba anaweza kuingia matatani baada ya kuonekana akiendesha gari huku akitumia simu kitu ambacho ni kinyume na sheria za uendeshaji gari nchini England.

MAMELODI SUNDOWNS FC WATUA DAR KUZIFUATA SIMBA, AZAM Msafara wa kikosi cha Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini umewasili leo Jumatatu mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka kambi kwa muda kisha kucheza mechi mbili za kirafiki. Mamelodi wamewasili Dar es Salaam wakiwa na jumlaya watu 42 huku ikielezwa kuwa wengine 10 wanatarajiwa kuingia kesho Jumanne. Ikiwa Dar es Salaam, Mamelod inatarajiwa kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa kisha dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex wiki hii kabla ya kuondoka Jumamosi ijayo.

DIMITRI PAYET JEURI SANA, AKAMILISHA DILI LA UHAMISHO, AWATOLEA KAULI WEST HAM Dimitri Payet ametangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Marseille ya Ufaransa akitokea West Ham United ya England kwa ada ya pauni 25m lakini kuna neno ametoa kuhusu timu yake ya zamani. Payet ambaye alitolewa lugha nyingi kali na mashabiki wa West Ham walimuona kama msaliti kwa kugoma kucheza akitaka auzwe amesaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu yake hiyo ya nyumbani na kuamua kuzungumzia kilichotokea. Akizungumzia kuhusu tabia yake iliyojitokea mpaka dili hilo linakamilika, Payet amesema: "Sina haja ya kuthibitisha au kufafanua kuhusu tabia yangu. Slaven Bilic (kocha wa West Ham) tulizungumza na tunajua kilichotokea. “Sina cha ziada kuzungumzia kuhusu suala hilo, naona bora nitahifadhi hayo, nitayazungumza siku nyingine lakini siyo sasa, kwa ufupi nilihitaji sana kurejea Ufaransa hasa Marseille."

HAWA WACHEZAJI WOTE WAMEZALIWA LEO NA MIAKA YAO WALIYOTIMIZA Wachezaji waliozaliwa leo na umri waliotimiza (kwenye mabano) Fili Djuricic (25) Dimitar Berbatov (36) Arda Turan (30) Lucas Biglia (31) Peter Crouch (36) Juninho (42) HERI YA KUZALIWA KWAO

Watoto wa baba mmoja wameipeleka Ghana nusu fainali AFCON 2017 Watoto wa baba mmoja Jordan Ayew na Andre Ayew kila mmoja alifunga goli kuichapa DR Congo 2-1 na kuihakikishia Ghana kucheza nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika. Jordan Ayew ambaye ni mshambuliaji wa Aston Villa alizifungua nyavu za DR Congo dakika ya 62 kwa kuuzungusha mpira ambao ulijaa moja kwa moja kwenye nyavu za goli la the Leopards. Paul-Jose M’Poku akaisawazishia DR Congo kwa mkwaju mkali akiwa nje ya box. Mshambuliaji wa West Ham Andre Ayew akafunga goli la ushindi kwa the Black Stars kwa mkwaju wa penati na kuifanya Ghana ifuzu moja kwa moja kucheza nusu fainali ya AFCON 2017. Ghana imefuzu kwa mara ya sita mfululizo kucheza nusu fainali ya michuano ya AFCON huku wakitafuta kumaliza ukame wa taji hilo walilolitwaa mara ya mwisho miaka 35 iliyopita.