pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 29 Novemba 2016
VIONGOZI SIMBA WAONA HII SASA NI KERO, WAAMUA KUACHANA NA MKUDE Katika siku za hivi karibuni kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye mkataba wake na timu hiyo unafikia tamati mwezi Januari mwakani, alisema kuwa mpaka sasa haelewi chochote kama ataendelea kuitumikia timu hiyo au la. Kutokana na hali hiyo, Mkude akawataka Yanga wakamsajili kama kweli wanamhitaji akidai bila kusita atasaini timu hiyo, kwani yupo tayari kuitumikia. Jambo hilo linadaiwa kuukera uongozi wa Simba na umeamua kuchukua jukumu la kukaa kimya bila ya kumfuatilia tena kiungo huyo na wamesema kama anataka kwenda Yanga aende. “Mkude hivi sasa anatakiwa kuwa makini sana, vinginevyo anaweza kujikuta katika wakati mgumu kwani uongozi umesema kuwa hautahangaika naye tena, yeye kama anataka kuondoka basi aondoke zake. “Wamefikia hatua hiyo baada ya kumbembeleza sana kusaini mkataba mpya lakini yeye amekuwa akizingua akidai kuwa fedha anazotaka kupewa ni kidogo lakini pia kila akiitwa kwa ajili ya mazungumzo amekuwa akikataa,” kilisema chanzo chetu cha habari na kuongeza: “Kutokana na hali hiyo uongozi wa timu unamsubiria kocha aje ili uweze kuzungumza naye na ikiwezekana aanze kuwa anamtumia Mzamiru Yassin kama kiungo mkabaji halafu Juma Awadh awe anacheza namba nane.” Alipotafutwa Mkude ili aweze kuzungumzia hali hiyo alisema: “Kama wamefikia uamuzi huo ni wao lakini binafsi kwa sasa siwezi kusema chochote juu ya suala hilo.”
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu wa ufukweni (beach soccer) Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer), John Mwansasu ameita kikosi cha wachezaji 12 kati ya 13 wanaotarajiwa kuivaa Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Desemba 9, 2016 utakaofanyika Dar es Salaam. Mwansasu ambaye hivi karibuni kikosi chake kilicheza na Ivory Coast katika michezo miwili ya kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio ni makipa ambao ni Rajab Galla na Khalifa Mgaya. Mabeki ni Roland Revocatus, Juma Ibrahim, Kashiru Salum na Mohammed Rajab wakati Viungo ni Mwalimu Akida, Ahmada Ali na Samwel John huku washambuliaji wengine wakiwa ni Kassim Kilungo na Talib Ally pamoja na Ally Rabbi ambaye ni Nahodha na Mshambulaji wa timu hiyo. Kocha John Mwansasu bado anafuatilia viwango vya wachezaji mbalimbali ili kujaza nafasi moja ya kipa kabla ya Desemba mosi, 2016 baada ya Kipa Juma Kaseja kutoa taarifa kuwa atakuwa na udhuru wakati nyota mwingine, Mohammed Banka aliyeripotiwa kuwa safarini nchini Afrika Kusini
Arsenal kuwakosa Giroud na Debuchy Mshambuliaji wa Arsenal Mfaransa Oliver Giroud ataukosa mchezo wa ligi dhidi ya Southampton na kuwa majeruhi. Nyota mwingine atakakosa mchezo huo ni beki Mathieu Debuchy anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa Debuch lifanyiwa vipimo lakini bado majibu hayatoka. Mshambuliaji Lucas Perez anatarajiwa kuanza baada ya kupona maumivu ya enka yaliyomuweka nje kwa wiki tano.
Hii ndio sababu ya El Classico kutoonyeswa Live ndani ya England. Habari zilitoka ni kwamba mechi pendwa ya El Classico haitaonekana Live kwenye Tv za England. Mechi hii itachezwa Dec 3 na kutokana sheria za kurusha matangazo live siku hiyo inafanya mechi hii isiruke Live ndani ya England. Sheria zinasema kwamba hairuhusiwi mechi yoyote kurushwa live kati ya 2:45pm na 5:15pm kwa siku hiyo. zaidi ya nchi 100 watashuhudia mechi hii ambayo inawahusisha mastaa Ronaldo na Messi. Sky Sport wataonyesha full mechi lakini watachelewa muda kidogo tofauti na kama inavyotokea live duniani kote. Rais wa La Liga alisem,“Mechi haitaonyeshwa Live ndani ya England kutokana na katazo lililo kwenye kurusha mechi live kwa muda huo. Tulikua na nafasi tatu kwa ajili ya mechi hii ambayo ni 1pm,4:15pm na 6:30pm. Baada ya kuongea na washauri wetu wametuambia tucheze kucheza 6pm itakua imechelewa sana kwa Asia na 1pm itakua mapema sana kwa America.” “So tumechagua 4:15. Uchaguzi wa muda ni muhimu kwa kujali idadi kubwa ya watu watakao kuwa affected. Asia na America ni muhimu kuzingatia kutokana na idadi kubwa ya watu na angala ni muda fair kwa kila mpenda soka duniani.” Mechi hii pia itawakutanisha makocha ambao waliwai kuwa wachezaji kwenye El Classico mechi za zamani
Ajali nane za ndege zilizokumba timu za spoti Kuanzia ajali ya ndege ya Munich ambayo iliangamiza mabingwa mara tano wa timu ya soka ya Italia, Torino na timu yote ya kuteleza kwenye theluji ya marekani, hizi ni baadhi ya ajali za ndege zilizokumba timu za spoti. Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Brazil ilianguka nchini Colombia Ndege iliyokuwa imebeba timu ya soka ya Brazil imeanguka wakati ilipokuwa ikikaribia mji wa Medellin nchini Colombia na kuwaua karibu watu wote 81 waliokuwa ndani yake. Ndege hiyo ilikuwa na wachezaji wa timu ya Chapecoense, waliokuwa safarini kwenda kucheza fainali ya mashindano ya kimataifa ya vilabu vya Amerika ya Kusini. Chapecoense ndicho klabu ya hivi punde kukumbwa na mkasa kama huo. Mikasa mingine inayokumbukwa ni: 1949 Il Grande Torino Mwezi Mei mwaka 1949 ndege iliyokuwa imeibeba timu ya Torino ilianguka eneo la milima karibu na Turin na kuwaua watu 31. Wakati huo timu ya "Il Grande Torino" ilikuwa klabu kubwa nchini Italia baada ya kupata ushindi mara tano. Kablu hiyo hikuweza kujikwamua kufuatia ajali hiyo ambayo iliangamiza karibu kikosi chote. 1958 Ajali ya Munich Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Manchester United ilianguka mjini Munich Ndege iliyokuwa imebeba timu cha Manchester United ambayo ilikuwa wakati huo ilijulikana kama "the Busby Babes" ilianguka ilipokuwa ikipaa wakati timu ilikuwa ikirudi kutoka mechi ya bara ulaya dhidi ya klabu ya Red Star Belgrade. Wachezaji 8 wa United na watu wengine 15 waliaga dunia. 1961 timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani Wanachama wote 18 wa timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani walikuwa miongoni mwa watu 73 waliokufa baada ya ndege yao kuanguka karibu na uwanja wa ndege wa Brussels wakati ilipokuw ikitua. Timu hiyo ilikuwa safarini kwenda mji wa Prague, huko Czechoslovakia, kushiri mashindano na dunia ambayo wakati huo yalifutwa. 1972 Alive Siku ya Ijumaa tarehe 13 Oktoba mwaka 1972, ndege iliyokuwa imebeba timu ya Old Christians ambayo na timu ya raga ya Uruguay, ilitoweka ilipokuwa safarini kutoka mji wa Montevideo kwenda Santiago nchini Chile. Manusura wa Old Christians walikutana nchini Chile miaka 30 baada ya ajali Miezi miwili baadaye jeshi la wanahewa wa Chile waliwapata manusura 14 kutoka kwa ajali hiyo. Wengine wawili walikuw wametembea kwa siku 10 kabla ya kukutana na wafugaji katika milima ya Andean. Mkasa huo ulindikwa kwenye vitabu na baadaye kutengenezwa vilamu ,ALIVE, iliyoeleza jinsi manusura walikula nyama ya binadamu kuepuka kufa njaa. 1979 FC Pakhtakor Tashkent Mwezi Agosti mwaka 1979 wanachama 17 wa timu ya soka la Pakhtakor Tashkent waliuawa wakati ndege yao iligongana na ndege ngingine katika anga ya Ukrain. Watu wote 178 waliokuwa ndani ya ndege zote mbili waliangamia. Timu zingine kwenye muungano ya usovieti zilichangia wachezaji wa klabu hiyo kukiwezesha kumaliza msimu. 1987 Alianza Lima Timu ya soka ya Alianza Lima, moja ya vilabu vyenye mafanikio makubwa zaidi ilikuwa ikirejea mjini Lima wakati ndege yao ilianguka kwenda baharini dakika chache kabla ya kutua Timu yote wa Alianza Lima iliyokuwa miongoni mwa watu 43 iliangamia. Ni rubani tu wa ndege hiyo aliyeweza kunusurika. 1993 Timu ya Soka ya Zambia Wanachama 18 wa timu ya taifa ya Zambia waliuawa wakati ndege ya jeshi la Zambia ilianguka karibu na Gabon tarehe 28 mwezi Aprili mwaka 1993, walikuwa wikielekea kucheza mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Senegal. Ripoti rasmi kuhusu mkasa huo miaka kumi baadaye ilitaja matatizo ya kimitambo kwenye injini moja ya ndege hiyo. 2011 timu ya magongo ya Lokomotiv Yaroslavl Timu hiyo ambayo ilikuwa ndio mabingwa mara tatu nchini Urusi ya Lokomotiv Yaroslavl, iliangamia kwenye ajali ya ndege mwezi Septemba mwaka 2011. Mabaki ya ndege yalipatikana kwenye mto uliokuwa karibu Ndege hiyo ilikuwa ikielekea nchini Belarus kwa mechi ya kwanza ya msimu wakati ilianguka na kushika moto. Wachezaji 36 na maafisa waliaga dunia pamoja na wahudumu 7. Mchezaji mwingine aliaga dunia akiwa hospitalini.
TFF YAWEKA MSISITIZO YANGA KUWALIPA TEGETE NA OMEGA SEME Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilikutana jana Jumapili Novemba 27, 2016 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia mashauri manane na moja wapo ni ile ya Yanga iliyokuwa ikidaiwa na wachezaji wake wa zamani na kusisitizwa kuwalipa. Shauri la 6. Malipo ya wachezaji Jerry Tegete, Omega Seme na Thabit Mohammed Kamati iliamua utekelezwa ufanyike kwa Klabu ya Young Africans kuwalipa wachezaji hao kama uamuzi ulivyokwisha kutoka hapo awali. TFF iandikie barua Young Africans kuhakikisha inawalipa. Shauri la 7. Madai ya Mchezaji Said Bahanuzi dhidi ya Young Africans. Suala la Bahanuzi limesogezwa mbele basi kwa kwa kuwa halikujadiliwa. Shauri la 8. Mchezaji Said Hussein Morald Mchezaji huyo kwa sasa ni huru baada ya yeye na Klabu ya Singida Unitedf kufikia mwafaka kwa barua ambazo waliwasilisha mbele ya kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.
SUALA LA KESSY LAINGIA KWENYE DANADANA, LAHAMISHIWA KAMATI NYINGINE ITOE MAAMUZI! Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilikutana jana Jumapili Novemba 27, 2016 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia mashauri manane. Shauri la 1. Klabu ya Simba dhidi ya Young Africans na mchezaji Hassan Hamis Ramadhani Kessy Shauri hili sasa limerudi rasmi kwenye meza ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji. Kamati iliyoketi chini ya Makamu Mwenyekiti, Mwanasheria Raymond Wawa imekubali shauri hilo kurejea kwenye Kamati yake na imeahidi kutoa maamuzi ndani ya wiki hii. Shauri la 2. Malalamiko ya Ayoub Nyenzi na wenzake Shauri hili pia limepangwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki hii. Uongozi wa Young Africans, umeagizwa kuleta nyaraka/kesi inayodai kuwa viongozi hao waliofukuzwa uanachama na Mkutano Mkuu wa dharura ama walishiriki au walifungua shauri mahakamani. Uongozi wa Young Africans, chini ya Kaimu Katibu Mkuu Baraka Deusdedit ulikubali kuwasilisha nyaraka hizo kabla ya kikao kijacho kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii. Wenzake na Nyenzi ni Hashim Abdallah na Salum Mkemi. Shauri la 3. Klabu ya Simba na Kocha Amatre Richard Kamati ilijikita kwenye hukumu yake na kuitaka Sekretarieti ya TFF kuandikia Simba kuhusu msimamo wa hukumu iliyotolewa kwa Simba kumlipa kocha huyo. Shauri la 4. Malalamiko ya Young Africans dhidi ya Kagera Sugar. Wahusika kwenye shauri hili, wameamuliwa kwenda Dar es Salaam mbele ya kikao kitakachoitishwa mwishoni mwa wiki ili kujieleza. Wahusika hao ni Young Africans waliowasilisha malalamiko, Panone FC ya Kilimanjaro, Kagera Sugar pamoja na mchezaji husika ili hatua stahiki zichukuliwe mara baada ya kuwasikiliza.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)