pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 1 Januari 2017
WEWE BISHA LOLOTE KUHUSIANA NA SCORPION KICK ZA MKHITARYAN NA GIROUD, LAKINI HUU NDIYO UKWELI Siku sita zilizopita, kiungo Henrikh Mkhitaryan wa Man United alifunga bao safi wakati timu yake ikivaa Sunderland. Bao hilo lilikuwa gumzo na kupewa jina la Scorpion Kick. Lakini siku sita baadaye unaweza kusema amepata jibu. Olvier Giroud wa Arsenal naye amefunga bao linalofanana na hilo katika mechi dhidi ya Crystal Palace ambayo Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 2-0. Sasa ni gumzo, kwamba bao hilo la Mhkitaryan raia wa Armenia na lile la Giroud kutoka Ufaransa. Lipi kali hasa? Kila mmoja anaweza kuwa huru kupitia maoni yake pamoja na ushabiki. Lakini ukweli ni hivi; bao la Mkhitaryan lilikuwa bora la funga mwaka 2016 na lile la Giroud limekuwa bora la fungua mwaka 2017.
ARSENAL YAIBOMOA CRYSTAL PALACE 2-0, GIROUD AKIMJIBU MKHITARYAN SCORPION KICK Arsenal (4-2-3-1): Cech 6.5; Bellerin 7, Gabriel 6, Koscielny 6.5, Monreal 5; Elneny 6.5 (Coquelin 72, 6), Xhaka, 6; Perez 6 (Ramsey 72, 6), Iwobi 8 (Oxlade-Chamberlain 77), Sanchez 7; Giroud 7.5 Substitutes not used: Ospina (GK); Mustafi, Reine-Adelaide, Maitland-Niles Manager: Arsene Wenger 6.5 Scorers: Giroud 17; Iwobi 56 Booked: Monreal Crystal Palace (4-2-3-1): Hennessey 7; Kelly 5, Tomkins 5, Dann 6, Ward 6; Flamini 5, Cabaye 5 (Mutch 65, 5); Townsend 6.5 (Lee 71, 5), Puncheon 5, Zaha 5; Benteke 6.5 (Campbell 77) Substitutes not used: Speroni (GK); Sako, Husin, Phillips Manager: Sam Allardyce 6 Booked: Tomkins Referee: Andre Marriner (West Midlands) 6 Attendance: 59,975
ALLI, KANE KILA MMOJA ATUPIA MBILI TOTTENHAM IKIITWANGA WATFORD 4-1 NA KUREJEA TOP FOUR WATFORD (3-4-3): Gomes 4; Cathcart 3.5, Kaboul 3.5, Prodl 3.5; Amrabat 4 (Sinclair 75, 5), Capoue 5.5 (Kabasele 79, 5), Guedioura 5.5, Holebas 4 (Mason 68, 6); Doucoure 4, Deeney 5.5, Ighalo 4 Substitutes not used: Pantilimon (GK); Stewart, Rowan, Folivi Manager: Walter Mazzarri 4 Scorer: Kaboul 90+1 Booked: Holebas, Prodl, Cathcart Tottenham Hotspur (3-5-2): Lloris 6; Dier 7, Wimmer 7, Alderweireld 7; Trippier 8, Wanyama 7.5, Alli 8 (Winks 61, 6.5), Eriksen 8, Rose 7.5 (Davies 68, 6.5); Kane 9 (Janssen 77, 6), Son Substitutes not used: Vorm (GK); Sissoko, Dembele, Carter-Vickers Manager: Mauricio Pochettino 8 Scorers: Kane 27, 33; Alli 41, 46 Referee: Michael Oliver (Northumberland) 6.5 Attendance: 20,882
BENCHI LA UFUNDI LA YANGA LATAKA MABAO ZAIDI, WACHEZAJI WAAMBIWA WAFANYE KAZI MAPINDUZI Benchi la ufundi la Yanga linaonekana kutoridhishwa na mabao yanayofungwa licha ya kwamba kikosi chao kinaongoza kwa ufungaji wa mabao. Katika mechi 18 Yanga imefunga mabao 39 na ndiyo inayoongoza kwa kufunga katika timu zote za Ligi Kuu Bara. Lakini Lwandamina amewaambia wachezaji wake anataka mabao zaidi na wanaweza kuanza kuonyesha kwenye michuano ya Mapinduzi. “Kocha kasisitiza sana suala la kutumia nafasi. Mechi na Lyon tulipoteza nafasi nyingi sana, tukaambulia sare. Mechi na Ndanda umeona tumerudi na kocha anataka hivyo au zaidi,” alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga. Benchi la ufundi, bosi mkuu ni Hans van der Pluijm ambaye ni mkurugenzi wa ufundi, kocha mkuu ni George Lwandamina raia wa Zambia.
NAKUKUMBUSHA ILICHOKISEMA TFF KUHUSIANA NA YULE MCHEZAJI ALIYETOKEA MBAO KWENDA LYON Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewataka wadau wa mpira wa miguu nchini wapuuze taarifa za kwenye mitandao kuhusu mchezaji Venance Ludovick. Suala la mchezaji huyo linaendelea kufanyiwa kazi na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji. Tunawahakikishia umma wa wapenda soka nchini kuwa haki itatendeka kwa mujibu wa kanuni zinazoendesha mashindano husika.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)