LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: SIMBA 3 VS 0 PRISONS (KIPINDI CHA PILI) SUB Dk 74 Pastory Athanas anaingia kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib
Dk 73, Prisons wanaingia vizuri na Meshack anauchonga vizuri mpira lakini unatoka nje kidogo mwa lango la Simba
Dk 73, pasi nzuri ya Mavugo, Kazimoto anaachia shuti kali hapa, lakini kipa anadaka
Dk 72, Ndemla anaachia shuti kali hapa lakini goal kick
SUB Dk 70 Shiza Kichuya anaingia kuchukua nafasi ya Liuzio
GOOOOOOO Dk 68, Mavugo anaifungia Simba bao la tatu kwa Kichwa akiunganisha krosi ya outer ya Ajibu
Dk 65 Chona wa Prisons naye yuko chini paleSUB Dk 62, Kazimoto anaingia kuchukua nafasi ya Mwanjale
Dk 62 Mwanjale anatolewa nje kwenda kutibiwa
Dk 61, Mwanjale yuko chini baada ya kuumia, inaonekana hataendelea kwani mara ya pili ndani ya dakika 5 anaanguka na kutibiwa
Dk 58, Agyei tena anaikoa Simba baada ya krosi dongo ya Kimenya
Dk 57, Krosi ya Bukungu ndani ya eneo la hatari lakini haikumfikia yoyote, Prisons wanaokoa
SUB Dk 56 upande wa Prisons Meshack Selemani anaingia kuchukua nafasi ya Benjamin Asukile
Dk 55, Mavugo anawatoka mabeki wa Simba, wanaokoa na kuwa kona, inachongwa lakini goal kick
Dk 54, Prisons wanaingia ndani ya eneo la hatari la Simba, Agyei anafanya kazi ya ziada tena
Dk 51, krosi nzuri ya Kimenya ndani ya lango la Simba, Agyei anatokea na kudaka kama nyani
Dk 49, Hamisi wa Prisons anageuka vizuri na kuachia mkwaju lakini unakuwa goal kick
Dk 47, Mwanjale anafanya kazi ya ziada kuokoa mbele ya Asukile aliyekuwa anakwenda kumuona Agyei, yuko chini anatibiwa sasa
Dk 45, kipindi cha pili kimeanza na kila upande unaonekana kuwa makini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni