LIVE KUTOKA MAJIMAJI SONGEA: MAJIMAJI 0-2 SIMBA GOOOOOOOOO Dk 64 Ndemla anaachia mkwaju mkali na kuiandikia Simba bao la pili. Ulikuwa ni mpira safi wa kona, Majimaji wakajichanganya naye hakufanya ajizi
Dk 63, Simba wanagongeana vizuri, Mavugo anampa Kotei anaachia shuti kali, linaokolewa na kuwa kona
SUB DK 60, James Kotei anaingia kuchukua nafasi ya Ajibu, mfungaji wa bao pekee hadi sasa
Dk 58, Mavugo anamchambua beki hapa, anaachia mkwaju lakini hakulenga langoDk 57 sasa, Majimaji ndiyo wanaoshambulia sana, Simba wanapaswa kuwa makini kwa kuwa inaweza kuwa hatari kwao
Dk 56, Kaheza, yeye na kipa anapiga lakini mpira wake unamgonga kipa na kwenda nje. Kona, inachongwa lakini haina faisa
DK 52, mpira mzuri wa Mavugo unaokolewa na kuwa kona, inachongwa na kuzaa kona nyingine
SUB Dk 52, Simba wanamtoa Juma Liuzio na nafasi yake inachukuliwa na Pastory Athanas
Dk 50, Sabato anajaribu kumtoka Mwanjale lakini anautoa na kuwa kona, inachongwa, Agyei anapangua na mabeki wanaondosha
Dk 49, Kibuta anageuka na kuachia mkwaju mkali kwa mara nyingine, lakini hakulenga lango. Goal kick
Dk 47 Simba wanagongeana vizuri kabisa hapa na Ajibu anaachia mkwaju mkali kabisa lakini sentimeta chache, goal kick
Dk 45, mechi imeanza kwa kasi na Simba wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Majimaji
MAPUMZIKO
Dk 45+1 shuti la mpira wa adhabu wa Kaheza, Agyei anatema na mabeki wake wanaokoa. Inakuwa kona lakini haina manufaa kwa Majimaji
DK 45+1, krosi nzuri kabisa, Kibuta yeye na kipa wa Simba, anafumba macho na kuukosa mpira
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 45, Majimaji wanaingia tena kwenye lango la Simba lakini Mwanjale anaokoa mbali kabisa
DK 44, nafasi nzuri kwa Majimaji, Sabato anaupata vizuri anapiga kichwa lakini anashindwa kulenga
DK 42 sasa, Majimaji wanaonekana kufunguka na kucheza vizuri lakini hawako makini sana wanapoingia kwenye lango la Simba
Dk 40, Kipangile wa Majimaji anaingia kwenye lango la Simba, lakini anashindwa kutulia
Dk 39, Selemani Kibuta mbele ya Muzamiru anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, unatoka pembeni kidogo ya lango la Simba
Dk 35, Mavugo anapokea pasi nzuri ya Ajibu na kupiga shuti kali, linatoka sentimeta chache kabisa
Dk 31, Sabato anaingia vizuri tena na kuachia shuti lakini hakulenga
Dk 28 Majimaji wanapoteza nafasu nzuri hapa na Agyei anadaka vizuri kabisa
Dk 22, Sabato anapoteza nafasi nzuri baada ya kuunganisha kichwa karibu na lango la Majimaji lakini hakulenga
GOOOOOOO Dk 19, krosi safi ya Shiza Kichuya, Ajibu anaunganisha vizuri kwa kichwa na kuandika bao la kwanza kwa Simba
Dk 15 sasa, Simba wanaonekana na kugongeana vizuri lakini bado hakuna kashkash kubwa wanayofikisha langoni
Dk 12, Kona ya pili wanapata Majimaji hapa baada ya Bukungu kuutoa mpira nje, inachongwa lakini Agyei anadaka
Dk 11 Simba wanagongeana vizuri na Liuzio anaupachika mpira wavuni. Mwamuzi anasema kabla, tayari alikuwa ameotea
DK 9, krosi inapigwa langoni mwa Simba, kipa Agyei anakwenda markiti lakini Zimbwe au Tshabalala anajitokeza na kuokoa vizuri kabisa
Dk 8, kona ya kwanza ya mchezo wanapata Majimaji baada ya Mwanjale kuutoa mpira kwa kichwa
Dk 7, Peter anageuka na kuachia mkwaju hapa lakini Agyei anadaka kwa ulaini
Dk 7 sasa, bado mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makubwa ndani ya
Dk 2 Simba wanaingia kwenye lango la Majimaji, Mazamiru anapiga shuti linawababatiza mabeki hapa na wanaokoa
Dk ya 1, Majimaji wanaanza kwa kasi, krosi nzuri inapigwa hapa lakini mwamuzi anasema offside
KIKOSI CHA SIMBA:
1. Daniel Agyei
2. Janvier Bukungu
3. Mohamed Zimbwe
4. Novatus Lufunga
5. Method Mwanjale (C)
6. Muzamiru Yassin
7. Shiza Kichuya
8. Said Ndemla
9. Laudit Mavugo
10. Juma Liuzio
11. Ibrahim Ajibu
SUB
Peter Manyika
Mwinyi Mazimoto
James Kotei
Haji Ugando
Athanas
Kitandu
04
Feb
2017
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni