Alhamisi, 5 Januari 2017

MPINZANI WA NAMBA WA SAMATTA AUMIA GOTI, ATAKUWA NJE MIEZI NANE MSHAMBULIAJI Mgiriki Nikolaos Karelis anayecheza nafasi moja na Mtanzania Mbwana Ally Samatta katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ameumia goti na atakuwa nje kwa miezi nane. Karelis aliumia mwishoni mwa mwaka katika mchezo dhidi ya KAA Gent Desemba 27, Uwanja wa Laminus Arena Genk ikishinda 2-0, tena yeye akifunga bao la pili dakika ya 26. Nikolaos Karelis anayecheza nafasi moja na Mbwana Samatta atakuwa nje kwa miezi nane Na baada ya kufanyiwa vipimo siku iliyofuata, ikagundulika Karelis ameumia vibaya goti la mguu wake wa kushoto na atahitaji kufanyiwa upasuaji, ambao utamuweka nje ya uwanja si chini ya miezi minane. Wakati Karelis akienda kwenye matibabu, KRC Genk sasa itamtegemea Samatta kwa kipindi chote hicho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni