pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 5 Januari 2017
Majibu ya Mayanja kama Simba itakutana na Yanga au Azam Mapinduzi Cup 2017 Simba, Yanga au Azam huenda zikakutana kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi kutokana na misimamo ya makundi yao. Simba inaongoza Kundi A ikiwa na pointi saba, Yanga yenyewe ni kinara wa Kundi B kwa pointi zake 6 wakati Azam ipo nafasi ya pili kwenye Kundi B nyuma ya Yanga ikiwa na pointi 4. Baada ya mchezo kati ya URA vs Simba, kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema timu yake ipo tayari kukutana na timu yeyote iwe Azam au Yanga. Mayanja anasema haya ni mashindano unaweza kukutana na timu yoyote mbele yako kwa hiyo unatakiwa kuwa tayari. “Yanga, Azam, zote zipo katika michuano ya Mapinduzi sisi hatuna tabu kwa sababu haya ni mashindano tunaweza kukutana na timu yeyote, kila timu tutakayokutana nayo tutapambana,” alisema Mayanja wakati akijibu maswali ya wanahabari. Lakini pia Mayanja akazungumzia kiwango cha Simba ambacho kinaonekana ni cha kupanda na shuka kwenye michuano ya Mapinduzi ukilinganisha na kilivyokuwa kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara. “Tumekuja kwenye Mapinduzi tukiwa tumetoka kucheza ligi kwa hiyo wachezaji wanauchovu halafu tunacheza kila baada ya siku moja kwa hiyo uchovu nao unachangia.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni