Alhamisi, 5 Januari 2017

Jang’ombe Boys inafata nyayo za Simba Mchezo wa Kundi A kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya KVZ umemalizika kwa vijana wa Jang’ombe Boys kupata ushindi wao wa pili kwenye michuano hii baada ya kuifunga KVZ kwa magoli 3-1. Abdul-samad Kassim Ali ndiye shujaa wa mchezo huo kwa sababu amekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga hat-trick. Kassim alifunga magoli yote katika kipindi cha kwanza huku bao lake la tatu likiwa ni la mkwaju wa penati. Jang’ombe Boys watacheza na Simba kwenye mchezo wao unaofuata wa Kundi A kabla ya kujua hatima ya timu gani itasonga mbele kucheza hatua ya nusu fainali. Salum Songoro Maulid ndiye aliyefunga bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa KVZ. Ushindi wa Jang’ombe Boys unaifanya timu hiyo kufikisha pointi 6 sawa na Simba ambayo saa 2:15 usiku itacheza na URA yenye pointi tatu ilizopata kwenye mchezo wake dhidi ya KVZ ambayo bado haijaambulia pointi hadi sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni