Jumanne, 3 Januari 2017

Jang’ombe Boys imepata ushindi kwa mabigwa watetezi Mapinduzi Cup Jang’ombe Boys imekuwa timu ya pili kutoka Zanzibar kupata ushindi kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2017. Boys wameifunga URA FC ya Uganda kwa magoli 2-1 na kuchukua pointi tatu muhimu ikiwa ni mechi ya pili kwa timu hizo zilizopangwa Kundi A. Magoli ya Jang’ombe Boys yamefungwa na Khamis Mussa ‘Rais’ dakika ya 16 na 31 wakati Labama Bogota akifunga bao pekee la URA huku likiwa ni bao lake la tatu kwenye mashindano. Awali Taifa Jang’ombe ndio ilikuwa timu pekee ya Zanzibar iliyopata ushindi kwa kuifunga Jang’ombe Boys kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano hii uliochezwa December 30. January 1 KVZ ambayo ni timu nyingine ya Zanzibar ilipoteza mchezo wake mbele ya URA kwa magoli 2-0. Azam FC wakaifunga 1-0 Zimamoto huku Yanga ikiishushia gharika Jamhuri kwa kipigo cha 6-0 na kuzifanya timu za Zanzibar zikishindwa kufurukuta kwa wageni wao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni