Azam wameihuzunisha tena Simba baada ya siku 15 Azam FC wamerudia kile walichokifanya Zanzibar kwenye fainali ya Mapinduzi Cup kwa kuitungua tena Simba kwa bao 1-0 kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa.
Goli pekee lililoipa Azam ushindi na pointi tatu limefungwa na nahodha John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 69 kipindi cha pili na kuimaliza Simba.
Ushindi kwa Azam unamaanisha Simba inaendelea kubaki na pointi 45 baada ya kucheza mechi 20 ikiwa mbele ya Yanga kwa pointi mbili pekee lakini ‘wakimataifa’ wanamchezo mmoja mkononi.
Endapo Yanga watapata ushindi kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Mwadui FC wataiondoa Simba kileleni kwani watafikisha pointi 47, lakini kama watapata sare ya aina yoyote watafikisha pointi 45 na kuwa sawa na Simba lakini bado Yanga wataongoza ligi kwa uwiano wa magoli.
Hadi sasa Yanga wana wastani wa magoli 31 wakati Simba wao wana wastani wa magoli 24.
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Simba kutoka kwa Azam ikiwa ni siku 15 zimepita baada ya timu hizo kukutana kwenye mchezo wa fainali ya Mapinduzin Cup ambayo ilichezwa January 13, 2017.
Kikosi cha Simba
Daniel Agyei, Javier Bokungu, Mohamed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjale, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Pastory Athanas, Said Ndemla, Jamal Mnyate na Juma Liuzio.
Kwenye benchi
Peter Manyika, Vicent Costa, Novalty Lufunga, Laudit Mavugo, James Kotei, Ibrahim Ajib, Shiza Kichuya
Kikosi cha Azam
Aishi Manula, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Yakub Mohamed, Himid Mao, Stephen Kingue,Frank Domayo, Ramadhan Singano, Joseph Mahundi na John Bocco
Kwenye benchi
Metacha Mnata, David Mwantika, Abdallah Kheri, Shabani Idd, Masoud Abdala, Mudathir Yahaya na Yahaya Mohammed.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni