LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: YANGA 4-0 NDANDA (FULL TIME) MPIRA UMEKWISHA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, Ndanda wanafanya shambulizi kali hapa, Dida anaokoa
GOOOOOOO Dk 88, Bossou anaiandikia Yanga bao la nne, likiwa ni bao la 39 la Yanga msimu huu katika Ligi Kuu Bara na la pili kwake msimu huu. Aliungainisha mpira wa kona
Dk 87, Yanga wanapata koa yao ya sita leo baada ya NGalema kuiwahi krosi ya MSuva. Ila Ngalema yuko chini pale
Dk 86, Yanga wanaendelea kutawala huku Ndanda wakiwa hawana matumaini hata ya kupata bao moja tu
Dk 83, Jeremiah, kipa wa Ndanda FC anaonyesha umahiri mkubwa kuokoa mpira wa kichwa wa Msuva akiunganisha krosi
Dk 80, Ndanda wanaingia vizuri, Kiggi anapiga krosi safi, kona. Hii ni kona ya pili ya Ndanda katika mechi hii, inachongwa na Mtama hapa, hakuna kitu
SUB Dk 78, Yanga wanamtoa Emmanuel Martin na nafasi yake inachukuliwa na Deus Kaseke
Dk 73, Omary Mponda anaachia mkwaju mkali kabisa hapa wa adhabu lakini Dida anadaka vizuri kabisa
SUB Dk 70, Thabani Kamusoko anaingia kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima
Dk 68, Yanga inaendelea kutawala mpira kwa asilimia kubwa
Dk 62, Yondani anaondoa mpira ndani ya eneo la 12 la lango lake lakini yeye na Rifat Hamisi wanaanguka. Wote wawili wanatibiwa hapa
SUB Dk 60 Yanga wanamtoa Said Juma 'Makapu' na nafasi yake inachukuliwa na Justice Zulu maarufu kama Mkata Umeme
Dk 55 sasa, inavyoonekana, Ndanda hawana shambulizi lolote kali langoni mwa Yanga.
SUB Dk 53, Abuu Ubwa anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Salum Mineli Dk 52, krosi nyingine safi ya Msuva, lakini Tambwe anajichanganya mwenyewe mpira ukiwa mguuni
Dk 51, krosi safi ya Niyonzima, anapiga krosi safi, Tambwe anapiga lakini mpira unatoka nje
Dk 49, Yanga wanapata kona, inachongwa vizuri kabisa hapa. Ngoma akiwa katika nafasi nzuri anapiga kichwa juuu
Dk 47, krosi safi ya Juma, Tambwe anaunganisha kichwa, Ndanda wanaokoa, mpira unakuta Martin anaachia shuti kali kabisa hapa, goal kick
Dk 46, mpira unaana na Yanga wanaonekana bado kuwa na uchu...
MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, Yanga wanafanya shambulizi jingine, safari hii Ngoma anapiga shuti, wanaokoa. Mwamuzi anasema ni offsise
Dk 44, Yanga wanafanya shambulizi kali, Msuva anaingia vziuri lakini Ndanda wanaokoa
SUB Dk 40 Ndanda wanamtoa Salvatory Ntebe na kumuingiza Ayoub Shabaan
Dk 39, Kipa Ndanda Jeremiah anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi kichwani mwa Tambwe
Dk 34, shuti kali la mpira wa adhabu la Kiggi, linadakwa kwa ulaiiniiii na Dida
Dk 32, Yanga wanagongeana vizuri tena, Mwinyi anampa Martin pembeni, anapiga krosi lakini mabeki Ndanda wanaokoa.
Dk 30 sasa, kipa wa Ndanda alikuwa anatibiwa kwa dakika mbili. Ameamka pale, mpira unarejea mchezoni
KADI Dk 26, Tambwe analambwa kadi kwa ushangiliaji wake usiokuwa wa kiungwana, aliruka na kukanyaga kibendera kikavunjika
GOOOOOOOO Dk 25, pasi safi, Tambwe anatulia na kuandika bao safi kabisa
Dk 24, Yanga wanagngena vizuri, Niyonzima anawachambua mabeki wa Ndanda na kuachia shuti kali, lakini kipa anadaka kama nyani
GOOOOOOOOO Dk 21, Ngoma anaandika bao la 37 kwa Yanga msimu, la pili kwake leo baada ya kuunganisha krosi safi kabisa kutoka kwa Juma Abdul ambayo ilimparaza beki wa Ndanda na kumfikia yeye aliyeupiga mpira na kutinga wavuni
Dk 19 sasa, Yanga inaendelea kupambana vizuri na mambo yanaonekana si mazuri kwa Ndanda
Dk 15, Ndanda wanapata kona yao ya kwanza, inachongwa na Ngalema, hatari hapa lakini Yanga wanaokoa
Dk 13, martin wa Yanga anaingia vizuri, anajaribu kupiga shuti lakini kipa wa Ndanda anaonyesha umahiri hapa
Dk 13, Kiggi Makasi anapiga mpira wa faulo, shuti kali kabisa hapa lakini Dida anadaka vizuri
Dk 9 sasa, kwa hali ilivyo, Ndanda wanalazimika kubadilika, la sivyo watafungwa tena, maana wanaachia upenyo kwa Yanga kupenya mara nyingi kwenye lango lao huku wao wakishindwa kabisa kumiliki mpira muda mrefu
Dk 8, Martin anawachambua mabeki wawili wa Yanga, anapiga krosi safi kabisa. Kidogooo, Tambwe anachelewa
Dk 5, Juma Abdul anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick
GOOOOOO Dk 4, Ngoma anaiandikia Yanga bao saafi kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona
Dk 1, mechi inaanza kwa kasi kubwa ikionekana Yanga wamepania kupata bao la mapema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni