LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: YANGA 3-0 NDANDA KADI Dk 26, Tambwe analambwa kadi kwa ushangiliaji wake usiokuwa wa kiungwana, aliruka na kukanyaga kibendera kikavunjika
GOOOOOOOO Dk 25, pasi safi, Tambwe anatulia na kuandika bao safi kabisa
Dk 24, Yanga wanagngena vizuri, Niyonzima anawachambua mabeki wa Ndanda na kuachia shuti kali, lakini kipa anadaka kama nyani
GOOOOOOOOO Dk 21, Ngoma anaandika bao la 37 kwa Yanga msimu, la pili kwake leo baada ya kuunganisha krosi safi kabisa kutoka kwa Juma Abdul ambayo ilimparaza beki wa Ndanda na kumfikia yeye aliyeupiga mpira na kutinga wavuni
Dk 19 sasa, Yanga inaendelea kupambana vizuri na mambo yanaonekana si mazuri kwa Ndanda
Dk 15, Ndanda wanapata kona yao ya kwanza, inachongwa na Ngalema, hatari hapa lakini Yanga wanaokoa
Dk 13, martin wa Yanga anaingia vizuri, anajaribu kupiga shuti lakini kipa wa Ndanda anaonyesha umahiri hapa
Dk 13, Kiggi Makasi anapiga mpira wa faulo, shuti kali kabisa hapa lakini Dida anadaka vizuri
Dk 9 sasa, kwa hali ilivyo, Ndanda wanalazimika kubadilika, la sivyo watafungwa tena, maana wanaachia upenyo kwa Yanga kupenya mara nyingi kwenye lango lao huku wao wakishindwa kabisa kumiliki mpira muda mrefu
Dk 8, Martin anawachambua mabeki wawili wa Yanga, anapiga krosi safi kabisa. Kidogooo, Tambwe anachelewa
Dk 5, Juma Abdul anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick
GOOOOOO Dk 4, Ngoma anaiandikia Yanga bao saafi kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona
Dk 1, mechi inaanza kwa kasi kubwa ikionekana Yanga wamepania kupata bao la mapema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni