LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: SIMBA 1 VS 0 JKT (MAPUMZIKO) MAPUMZIKO
-Wachezaji wa JKT wanaonekana kumzonga mwamuzi hapa wakilalamika kwamba kipa wao alikuwa chini
-Kipa bado yuko chini anatibiwa na mwamuzi akiwa anasubiri, anainuka hapa
GOOOOOOOOO DK 45+2, Muzamiru anaifungia Simba bao akiunganisha krosi ya Athanas, wakati huo kila Seif alikuwa chini baada ya kugongwa, hakuinuka
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 44, Kipa Hamisi Seif wa JKT, mwenyewe anakwenda hadi chini na kukaa. Sasa anatibiwa
Dk 43, Simba wamefanya shambulizi mfululizo kwa dakika moja nzima lakini JKT wamekuwa makini kuokoa, kipa wao wao Hamisi Seif anakuwa makini zaidi
Dk 38, Simba wanahamia kwenye lango la JKT, wanafanya mashambulizi matatu mfululizo lakini JKT wanaonekana wako makini kuokoa
DK 36, JKT wanafanya shambulizi jingine kali lakini shuti la Juma halikulenga lango
Dk 33, krosi safi inamkuta Kichuya, anajaribu shuti baiskeli lakini mpira unatoka nje
Dk 32, JKT wanapata kona baada aya kufanya shambulizi la kushitukiza, inachongwa na Mussa Juma, mpira unamkuta Mkude anaokoa
Dk 29, kipa wa JKT yuko chini baada ya kuumizwa, anapatiwa matibabu huku Simba wakisubiri kupiga kona
Dk 27, Simba wanapata kona ni baada ya kuendelea kupeleka presha kubwa kwenye lango la JKT
Dk 23, kipa Hamisi Seif anaokoa kwa ukaribu shuti la Muzamiru baada ya krosi safi ya Pastory
Dk 22 sasa, JKT wanabaki nyuma kwa wingi, wakiacha mtu mmoja tu na wanafanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 21, JKT wanafanya kazi ya ziada kuwazuia Simba baada ya kugongeana vizuri wakiingia kwenye lango lao
KADI Dk 20 Kotei naye analambwa kadi ya njano kwa kufanya madhambi
KADI Dk 19 Edward Joseph analambwa kadi ya njano kwa kubaki na mpira baada ya filimbi
Dk 17, Athanas anaingia vizuri hapa na kupiga shuti, beki wa Yanga anazuia na kipa anadaka vizuri
KADI Dk 15, Salim Aziz Gilla analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Athanas
Dk 11, Joseph wa JKT anaonyesha uwezo mkubwa kwa kuachia shuti kali lakini kipa Agyei anaonyesha umahiri kwa kuokoa na kuwa kona, isiyo na matunda
Dk 7, Pastory anajaribu vizuri hapa akiunganisha pasi ya Kichuya lakini shuti lake halikulenga lango
Dk 5 sasa, Simba wanaendelea kupanga mashambulizi lakini bado mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja
Dk 2, Banda anapiga vizuri hapa mpira wa adhabu, lakini kipa JKT anaonyesha umakini mkubwa
Dk 1, Pastory alikuwa anaondoka lakini anaangusha na kuwa faulo
Dk 1, mechi inaanza kwa kasi ikionyesha kila timu imepania kupata bao la mapema, JKT ndiyo wanaanza mpira na Simba wanafanya madhambi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni