LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: AFRICAN LYON 1 VS 0 YANGA (KIPINDI CHA PILI) Dk 62, Yanga wanapata kona nyingine, inachongwa akini mwamuzi anasema hapa, kulikuwa na mpira mwingine ndani ya uwanja
Dk 61, Yanga wanapata kona ya pili kipindi hiki na ya saba katika mchezo huu, inachongwa na Msuva, Tambwe anajitwika tena, lakini hajalenga
Dk 61, krosi ya Juma Abdul, Tambwe anajitwika lakini ni mpira rahisi kwa kipa huyu Mcameroon
GOOOOOOOOO Dk 59, Venance Ludovick aliyeingia kipindi cha pili anaifungia Lyon bao safi kabisa akiunganisha krosi maridadi kabisa
SUB Dk 58, Yanga wanamtoa Kamusoko na nafasi yake inachukuliwa na Obrey Chirwa raia wa Zambia
Dk 55, Tambwe katikati ya mabeki anaunawa mpira wakati Yanga ikishambulia. Kiasi fulani Yanga wanaongeza kasi ya mashambulizi
Dk 53, krosi safi ya MWinyi Haji, MSuva anajituma na kujitwika kichwa hapa, goal kick
Dk 50, Lyon wanapata mpira eneo si mbali na eneo la Yanga, anachonga Miraji Adam lakini anapiga buuuu
Dk 47, Juma Abdul tena anaachia shuti kali, linapita juu ya lango la Lyon
Dk 46, krosi safi ya Juma Abdul kwenda kwa Kamusoko lakini Lyon wanaokoa na kuwa kona
DK 46, Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Lyon, lakini ni goal kick
SUB Dk 46, Venance Ludovick anaingia kuchukua nafasi ya Awadhi Juma ambaye inaonekana atakuwa aliumia mwishoni mwa kipindi cha kwanza
KADI Makapu anapambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Awadhi Juma
-Sasa ni dakika ya 45+5, Niyonzima anajaribu shuti kali kabisa, lakini mpira unatoka juu. Yanga wanaonekana kuonana vizuri lakini wanashindwa kuipita ngome ya Lyon
MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, kona inachongwa safi, Bossou anaruka na kumgonga kipa wa Lyon, yuko chini hapa anatibiwa na wachezaji wa Lyon wanamvaa Bossou
Dk 44, MSuva anapiga mpira unamgusa mlinzi wa Lyon, kona. Inachongwa, Lyon wanaokoa tena, kona
Dk 44, krosi nzuri ya Kaseke, mpira unamfikia Kamusoko lakini Lyon wanaokoa hapa
Dk 39, krosi nzuri ya Niyonzima, MSuva anapiga kichwa safi hapa, kipa anajitahidi kuokoa na mwamuzi anasema ni offside
Dk 37 sasa, ndani ya dakika nne, Lyon wamefika kwenye lango la Yanga mara tatu, inaonekana wanazidi kuongeza mashambulizi taratibu
Dk 31, Mguhi yuko chini pale, anaonekana atakuwa ameumia baada ya kupiga kichwa ule mpira
Dk 30, Lyon wanafanya shambulizi zuri hapa, Mguhi anapiga kichwa safi lakini mpira wake haukulenga lango
DK 29 sasa, bado mpira unachezwa zaidi katikato ya uwanja na mashambulizi dhaifu ndani ya 18 kwa kila upande
KADI Dk 28, Bossou naye analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Abdallah Mguhi
KADI Dk 24, Manzi analambwa kadi ya njano kwa kumgonga Niyonzima
Dk 22, Yanga wanaingia vizuri, Juma anapiga krosi safi, wanaokoa Lyon na kuwa kona. Inachongwa lakini haina madhara
Dk 21 sasa, inaonekana Yanga imeshindwa kuifungia difensi ya Lyon ambayo imejaza zaidi ya walinzi wanne na viungo watatu nyuma ya mpira
Dk 19, mpira wa adhabu wa Juma Abdul, unamkuta Bossou anapiga kichwa kisicholenga lango, goal kick
Dk 17, Lyon wanaonekana kuanza kufanya mashambulizi madogomadogo ya kushitukiza
Dk 16, Dida anafanya kazi nzuri ya kuruka na kuudaka mpira wa Abdallah Mguhi
Dk 11, shambulizi la kwanza la Lyon langoni mwa Yanga, krosi nzuri kabisa lakini Yanga wanaokoa vizuri kabisa
Dk 8 sasa, bado mpira unaendelea kuchezwa zaidi katikati ya uwanja
Dk 5, Hassan Isihaka yuko chini pale anatibiwa baada ya kugngana na Tambwe
Dk 3, Niyonzima anatoa pasi nzuri kwa Juma Abdul, anapiga krosi nzuri lakini Tambwe anapiga kichwa kinachopaa mpira unapaa juuu
Dk 1, mechi imeanza na Yanga ndiyo wanaonekana kupania kupata bao la mapema, lakini Lyon wameanza wengi zaidi wakiwa nyuma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni