LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: AFRICAN LYON 0 VS 0 YANGA DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, kona inachongwa safi, Bossou anaruka na kumgonga kipa wa Lyon, yuko chini hapa anatibiwa na wachezaji wa Lyon wanamvaa Bossou
Dk 44, MSuva anapiga mpira unamgusa mlinzi wa Lyon, kona. Inachongwa, Lyon wanaokoa tena, kona
Dk 44, krosi nzuri ya Kaseke, mpira unamfikia Kamusoko lakini Lyon wanaokoa hapa
Dk 39, krosi nzuri ya Niyonzima, MSuva anapiga kichwa safi hapa, kipa anajitahidi kuokoa na mwamuzi anasema ni offside
Dk 37 sasa, ndani ya dakika nne, Lyon wamefika kwenye lango la Yanga mara tatu, inaonekana wanazidi kuongeza mashambulizi taratibu
Dk 31, Mguhi yuko chini pale, anaonekana atakuwa ameumia baada ya kupiga kichwa ule mpira
Dk 30, Lyon wanafanya shambulizi zuri hapa, Mguhi anapiga kichwa safi lakini mpira wake haukulenga lango
DK 29 sasa, bado mpira unachezwa zaidi katikato ya uwanja na mashambulizi dhaifu ndani ya 18 kwa kila upande
KADI Dk 28, Bossou naye analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Abdallah Mguhi
KADI Dk 24, Manzi analambwa kadi ya njano kwa kumgonga Niyonzima
Dk 22, Yanga wanaingia vizuri, Juma anapiga krosi safi, wanaokoa Lyon na kuwa kona. Inachongwa lakini haina madhara
Dk 21 sasa, inaonekana Yanga imeshindwa kuifungia difensi ya Lyon ambayo imejaza zaidi ya walinzi wanne na viungo watatu nyuma ya mpira
Dk 19, mpira wa adhabu wa Juma Abdul, unamkuta Bossou anapiga kichwa kisicholenga lango, goal kick
Dk 17, Lyon wanaonekana kuanza kufanya mashambulizi madogomadogo ya kushitukiza
Dk 16, Dida anafanya kazi nzuri ya kuruka na kuudaka mpira wa Abdallah Mguhi
Dk 11, shambulizi la kwanza la Lyon langoni mwa Yanga, krosi nzuri kabisa lakini Yanga wanaokoa vizuri kabisa
Dk 8 sasa, bado mpira unaendelea kuchezwa zaidi katikati ya uwanja
Dk 5, Hassan Isihaka yuko chini pale anatibiwa baada ya kugngana na Tambwe
Dk 3, Niyonzima anatoa pasi nzuri kwa Juma Abdul, anapiga krosi nzuri lakini Tambwe anapiga kichwa kinachopaa mpira unapaa juuu
Dk 1, mechi imeanza na Yanga ndiyo wanaonekana kupania kupata bao la mapema, lakini Lyon wameanza wengi zaidi wakiwa nyuma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni