SIRI IMEFICHUKA, KLABU YAMUAHIDI MESSI EURO MILIONI 100 ASISAINI MKATABA MPYA NA BARCELON Wakati mkataba wa nyota Lionel Messi unatarajia kufikia mwisho mwaka 2018, kuna klabu ambayo imetoa ofa ya day la usajili la euro million 100 litamlipa mshambuliaji huyo.
Sharti ambalo klabu hiyo imetoa ni Messi kutosaini mkataba mpya na Barcelona na badala yake imeweka mezani fedha hizo ambazo itamlipa Messi.
Gazeti la El Mundo la Hispania ndiyo limeandika habari hiyo lakini halijaeleza klabu hiyo ni ipi.
Tayari kulikuwa na taarifa kwamba Barcelona inataka kumuongezea Messi mkataba mpya, lakini inaonekana klabu nyingine zinataka Messi aondoke Barcelona nazo zip ate huduma yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni