pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 22 Novemba 2016
Simba haijaacha wala haijasajili mchezaji – Manara Klabu ya Simba SC imesema haijaacha mchezaji yeyote wala kusajili mchezaji yeyote hadi sasa, kama wakifanya hivyo watatoa taarifa rasmi kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wao. Msemaji wa Simba Haji Manara amesema wapenzi wa Simba wazipuuze taarifa zinazoandikwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari, taarifa zote za usajili ndani ya Simba hazitafichwa kama itatokea mchezaji ameachwa au kusajiliwa. “Simba haijamuacha mchezaji yeyote na haijamsajili mchezaji yeyote mpaka dakika hii, chochote kilichoandikwa kwenye mitandao ya kijamii na magazeti hivi sasa, kinachoandikwa na kitakachoandikwa bila kufuata authority kutoka kwetu (Simba) basi ni uongo,” amekanusha Manara baada ya taarifa kuzagaa kwamba klabu hiyo imeshakamilisha usajili wa mchezaji wao wa zamani Emanuel Okwi. “Sisi suala la usajili hatutaficha, tukimuacha mtu hatutaficha na tukimsajili mtu pia hatutaficha. Hatuna sababu ya kuficha, vinavyoandikwa hivi sasa ni uongo mtupu.” Jana Jumatatu November 21, zilienea pia taarifa za mchezaji wa klabu hiyo Abdi Banda kuachana na Wekundu wa Msimbazi ikiwa ni taarifa iliyoandikwa na mchezaji mwenyewe (Banda) kupitia ukurasa wake wa Instagram. Manara pia amekanusha taarifa hiyo kwa kusema Banda huenda alikuwa akijifurahisha kwasababu anajua bado anamkataba na Simba na klabu bado inamalengo nae. “Nimeona baada ya kutumiwa, lakini mimi sio msomaji wa mitandao ya kijamii, Simba haifanyi kazi kupitia mitandao ya kijamii.” Kama kweli ameaga angeaga kwa utaratibu sahihi, lakini anaagaje wakati bado anamkataba na Simba? Sasa mtu anaaga kupitia Instagram mimi najibu nini? Najibu kuhusu mambo ya Instagram ambayo kila siku yanaandikwa mapya? Tuachane na vitu kama hivyo, kama kaandika basi kajifurahisha kwasababu anajua bado anamkataba na Simba na hatutamwacha.” Utafiti uliofanywa na mompondazy. Blogspot.com umebaini ni kweli mchezaji huyo yuko mbioni kuondoka kwenye klabu hiyo iliyomsajili akitokea Coastal Union lakini hakuwa tayari kuweka wazi ni wapi anaelekea.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni