Rekodi zilizowekwa baada Chelsea ya kupaa kileleni Ushindi wa bao 1-0 iliopata Chelsea ugenini dhidi ya Middlesbrough uliiwezesha Chelsea kupata pointi tatu na kupanda kileleni kwenye msimamo wa Premier League baada ya kufikisha jumla ya pointi 28.
Bao pekee la Chelsea lilifungwa na Diego Costa dakika ya 41 kipindi cha kwanza na kudumu kwa dakika zote zilizosalia.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte amefanikiwa kuijenga vyema Chelsea baada ya kuanza msimu vibaya kwa kupewa vichapo kutoka kwa Liverpool na Arsenal.
Rekodi zilizowekwa baada ya mchezo wa Middlesbrough vs Chelsea
Chelsea imeshinda mfululizo mechi sita za Premier League bila kuruhusu goli ikiwa ni mara ya 10 kutokea ndani ya EPL lakini ni mara ya tano kwa Chelsea.
Diego Costa ni mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 10 kwenye Premier League katikamsimu huu.
Costa amefunga magoli sita katika mechi saba za ugenini, amefunga magoli saba katika mechi saba.
Swansea pekee imepata pointi chache (pointi mbili) katika mechi zake za nyumbani za Premier League ikifuatiwa na Middlesbrough (pointi nne).
Winger wa Middlesbrough Adama Traore ali-dribble mara 12 kwenye mchezo huo mara nyingi zaidi ya mchezaji yeyote kufanya hivyo kwenye mchezo mmoja ndani ya Premier League msimu huu.
Chelsea wananafasi ya kuendelea kufanya vizuri kwasababu hawashiriki katika mashindano mengi kwahiyo inaweza kuwa nafasi kwao ya kujikita zaidi kwenye ligi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni