Jumatano, 2 Novemba 2016

LIVE KUTOKA SOKOINE MBEYA: MBEYA CITY 2 VS 1 YANGA (KIPINDI CHA PILI)

Dk 46, Yanga wanaanza kwa kasi kubwa na kupata kona, inachongwa hapa, shuti kali hapa lakini unatoka nje, goal kick...kipa wa Mbeya City yuko chini anatibiwa MAPUMZIKO GOOOOOOOO Ngoma anaunganisha krosi ya Msuva vizuri hapa na kuandika bao moja kwa Yanga -KADI Mbuyu Twite analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ally Ramadhani DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 44, hakuna matumaini kama Yanga wanaweza kusawazisha dhidi ya Mbeya City kwa kuwa hakuna shambulizi kali Dk 42, mwamuzi anasema lile ni bao lililofungwa na Kenny Ally dak ya 36, hivyo Mbeya City wanaongoza kwa mabao 2-0 Dk 41 sasa, bado mpira umesimama na wachezaji Mbeya City wamekwenda kuwapumzisha mashabiki wao Dk 35, Mbeya City wanaukwamisha mpira wavuni baada ya Kenny Ally kuukwamisha wavuni, Mwamuzi akaonyesha ni bao, halafu akabadilisha lakini mwamuzi anasema kuwa walicheza kabla ya filimbi. Mashabiki na wachezaji Mbeya City naona wanaonyesha hasira hapa, askari wanalazimika kuanza kuzuia vurugu hivi, mpira umesimama sasa Dk 32, Raphael Alfa wa Mbeya City anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini Dida anaonyesha ujuzi na kupangua, kona. Yanga wanaokoa Dk 28, Shamte anaachia 'bunduki' kali mpira wa adhabu, safari hii Dida anadaka kwa ustadi mkubwa Dk 26, Msuva anaachia mkwaju safi hapa lakini kipa Mbeya City anapangua na kuwa konaaaa, inachongwa hakuna majibu mazuri Dk 22, City wanagongeana vizuri tena, Mahundi hatari huyu, anaachia shuti kaliii, hatari kabisa unatoka sentimeta chache kabisa kwenye lando la Yanga Dk 21, Yanga wanagongenaa vizuri hapa, mpira unamfikia Msuva anaachia fataki....wapiii Dk 19, kipa wa Mbeya City anaokoa mpira hatari wa Donald Dombo Ngoma SUB Dk 19 upande wa Mbeya City, Hemed Mlutabozwa anatoka baada ya kuumia, anaingia Hemed Ramadhani. Dk 15, Mbeya City nao wanapata kona baada ya krosi ya Maundi kuokolewa na kutoka. Mwasapili ndiye anachonga hapaa, Yanga wanaokoa Dk 14, Msuva anamtoka Mwasapili, krosi safi kabisa lakini City wanaokoa na kuwa kona ya pili Dk 13, Msuva anaingia vizuri na kupiga krosi, inaokolewa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina matunda Dk 11 sasa, bado Yanga wanaonekana hawajatulia wala kufanya shambulizi kali linaloweza kuwapa City presha GOOOOOOO Dk 6, Hassan Mwasapili anapiga mpira unaojaa moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa Dida Munishi Dk 1, kila timu imeanza taratibu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini hakuna inayocheza kwa papara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni