Jumatano, 2 Novemba 2016

LIVE KUTOKA KAMBARAGE SHINYANGA; STAND UNITED 0 VS 1 SIMBA (FULL TIME)

MPIRA UKWISHAAAAA -Mnyate anaachia shuti la chinichini hapa lakini ni goal kick -Mpira unateleza na unaonekana kuwasumbua wachezaji wengi -Simba wanaonekana kuosha kila mpira unaokwenda langoni mwao DAKIKA 6 ZA NYONGEZA Dk 89, Simba wanapata kona na inakwenda kuchongwa Bukungu, kipa Frank Muonge anajitahidi kudaka vizuri kabisa SUB Dk 88, Ibrahim Ajibu anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo Dk 88, mvua imeanza kunyesha uwanjani hapa na mashabiki wengi wanakimbia kutoka majukwaani Dk 87, Angban yuko chini baada ya kuumia wakati akijaribu kuudaka mpira wakati wa shambulizi lililoelekezwa langoni mwake Dk 82, kipa Muhonge anatoka na kumuwahi Mavugo aliyekuwa anakaribia kufunga. Lakini anampiga na mguu tumboni wakati akiokoa Dk 81, Mavugo anapokeza nafasi mujarab ya kufunga kwa kuwa kipa wa Stand alikuwa ametoka langoni, likiwa wazi MAvugo amepiga nje SUB 80, Moussa Ndusha ambaye ITC yake imekuja, anaingia kuchukua nafasi ya Kazimoto SUB Dk 75 Kichuya anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate DK 70, Wanachofanya Simba, wote wamerudi nyuma na wanafanya mashambulizi kwa kuwatumia watu watatu waende mbele kushambulia ambao ni Kichuya, Mavugo na Mwinyi Kazimoto tu Dk 67, Kiemba anafanya yake hapa, anamtoka Bukungu na Juuko na kutoa pasi safi Dk 64, Mo Ibrahim anaingia vizuri, ananyoshaa, unapita juu kidogo DK 60, Selembe anapiga kichwa safi mbele ya mabeki wa Simba, goal kick Dk 58, Stand wanapata kona inachongwa na Angban anaidaka kwa ulaini kabisa Dk 56, Job analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa pasi nzuri ya Kichuya iliyokuwa inakwenda kwa Mo Ibrahim. Inakuwa inachongwa lakini haina faida Dk 53, Stand wanafanya shambulizi kwa mpira wa adhabu, lakini juuuu Dk 50, Stand wanaonekana kwenda taratibu na zaidi wanamtumia Amri Kiemba ambaye yuko vizuri Dk 47, mpira umeanza kwa kasi na Stand United wanaonekana wamepania kusawazisha bao DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 45, Kichuya anapaa kama mkizi na kuunganisha kichwa mpira wa adhabu lakini unatoka sentimeta chache kwenye lango la Stand Dk 43, hakuna shambulizi kali zaidi ya kila timu kupiga pasi nyingi, Stand wakionekaan kufika zaidi kwenye lango la Simba Dk 42 sasa, Stand wanaonekana kuongeza mashambulizi mengi zaidi ya Simba ambao wanafanya mashambulizi ya kushitukiza tu Dk 35, Stand wanapata kona baada ya kusukuma mashambulizi mfululizo kwenye lango la Simba ]Dk 33, GOOOOOOOOO Kichuya aaukwamisha mpira wavuni Dk 31, PENAAAAAAAT...MAVUGO Anaangushwa na Adeyum Dk 30, Stand wanafanya shambulizi kali hapa, piga nikupige lakini Simba wanaokoa KADI Dk 29, Mwanjale analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Sabato Dk 27, mpira unaendelea lakini ni taratibu kutoka kila upande kama vile hakuna timu yenye haraka Dk 26 sasa, mpira umesimama, kuna mchezaji wa Stand United anatibiwa pale uwanjani Dk 23, Mo Ibrahim anapoteza nafasi nzuri hapa ya kufunga akiwa amebaki na lango, mpira unamzidi nguvu Dk 22, mpira unaonekana kuchezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali kwenye milango DK 19, Bukungu anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Kelvin Sabato Dk 13, Stand wanaonekana ni wengi zaidi nyumba huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza Dk 10, mpira unaonekana kuwa wa juu zaidi na hata milango haina kashkash sana, kila timu iko makini kwenye ulinzi Dk 5 sasa, bado mpira unaonyesha kuchangamka lakini timu zote mbili si bora katika umaliziaji Dk 1, mechi inaanza na Simba wanakuwa wa kwanza kushambulia. Lakini Mavugo anacheza faulo na mwamuzi anasema mpira uelekezwe Simba

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni