Jumapili, 2 Oktoba 2016

AFRICON 2017' SERENGETI BOYS YAPASUA, YAFUZ KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KWA KUIZUA CONGO KWAO

Pamoja na figisu rundo, timu ya taifa ya vijana, Serengeti Boys imefuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika itakayofanyika nchini Madagascar, kesho. Serengeti Boys wamefuzu baada ya sare ya bila mabao dhidi ya wenyeji wake Congo ya Brazzaville katika mechi iliyochezwa leo. Ilionekana wazi Wacongo walipania kufuzu licha ya kuwa wametoka Dar es Salaam na kipigo cha mabao 3-2. Lakini vijana wa Serengeti Boys wanaonolewa na Bakari Shime walionekana wako makini na mara kadhaa walifika kwenye lango la wapinzani wao na kutoa kashkash kubwa. Serengeti Boys ambao wanasonga kwa ushauri mkubwa wa Kocha Kim Poulsen, walionyesha soka zuri na la kisasa na kuwapa wakati mgumu Wacongo hao wanaoaminika kuwa na vijeba rundo. Sasa Serengeti Boys inakwenda Madagascar mwakani katika michuano ambayo itakuwa nafasi kuwakuza zaidi kwa kuwa watakutana na timu mbalimbali zenye mafanikio kisoka katika nyanja za vijana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni