KAZI NI KWENU VIJANA WA ILALA (U-17) JUMAMOSI HII JMK PARK
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Jumamosi hii (Septemba 3) itaendelea na programu ya majaribio ya wazi yenye lengo la kusaka vijana wenye vipaji chini ya umri wa miaka 17 (U-17).
Zoezi la kwanza ililolifanya kwa vijana wa Wilaya ya Temeke na Kigamboni, Azam FC iliweza kuvuna vijana watano bora kati ya 423 waliojitokeza kujaribiwa.
Kama umezaliwa mwaka 2000, 2001 au 2002 na unaishi Wilaya ya Ilala, unaombwa kufika na kuonyesha kipaji chako kwenye majaribio ya pili yatakayoanza saa 1.00 Asubuhi hadi saa 9.30 Alasiri kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete Park (JMK Park).
Tafadhali tunaomba kwa vijana wote watakaojitokeza, waje wakiwa na nakala za vyeti vyao vya kuzaliwa pamoja na wazazi au walezi wao.
Kwa majaribio mengine ya wazi katika maeneo mengine tutakayotembelea, tutawatangazia kwa siku za mbeleni kuhusu eneo, siku na muda.
Unaombwa kuwajulisha marafiki zako wote pale tu utakapopata taarifa hii.
Azam FC, iko katika kuleta mapinduzi kwa soka la Tanzania.
‘Timu Bora, Bidhaa Bora’ …
Akhanteni sana!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni