Ijumaa, 10 Machi 2017

AZAM FC WAWAOMBA SIMBA WAKAWASHANGILIE YANGA UWANJA WA TAIFA Uongozi wa Azam FC umewaambia wapenzi na mashabiki wa Simba na timu nyingine, waungane kwa pamoja kuishabikia Yanga, kesho Jumamosi itakapocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd huku akisisitiza kwamba kufanya hivyo ni uzalendo ambao unatakiwa kuanzia sasa na kuendelea. Yanga itacheza dhidi ya Zanaco katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mshindi atacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo. Upande mwingine, Azam FC yenyewe itacheza dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, keshokutwa Jumapili. “Kwa sasa lazima tukubali tu kwamba Yanga na Azam ndiyo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, hivyo litakuwa jambo la busara kwa mashabiki wote kuweka itikadi zetu pembeni na kuuungana pamoja kuhakikisha timu hizi zinafika mbali. “Nawaomba tu mashabiki wote, wa Azam, Simba na timu nyingine Jumamosi tukaishangilie Yanga pale Taifa, kisha Jumapili, tuungane tena kwenda Azam Complex kuishangilia Azam,” alisema Idd.

MAOFISA WA TFF WASHINDA SAKATA LA RUSHWA MAHAKAMA YA KISUTU Maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wameshinda kesi yao ya tuhuma za rushwa. Juma Matandika ambaye ni Msaidizi wa Rais wa TFF Jamal Malinzi, na Martin Chacha aliyekuwa mkurugenzi wao mashindano wa TFF. walikua wananashtumiwa kuomba rushwa ya milioni 25 kwa viongozi wa timu ya Geita Gold Sports ameachiwa huru Leo Sauti ziliolewa kuwa ni zao, zilisikika zikieleza mipango ya kuisaidia Geita Gold Sports na ilitakiwa fedha kwa ajili pia ya kuwapa viongozi wengine. Ingawa wadau wengi wanaojua sauti zao waliamini ni wao kabisa, lakini Mahakama ya Mkazi Kisutu imetupilia mbali ushahidi wa sauti uliowasilishwa mahakamani hapo.

Jumanne, 14 Februari 2017

ARSENAL ILIVYOIFUATA BAYERN NA KUMBUKUMBU YA KIPIGO CHA MABAO 5-1 Arsenal leo ina kibarua cha Ligi ya Mabingwa Ulaya itakapowavaa Bayern Munich ambao mara ya mwisho waliwatwanga kwa mabao 5-1. Tayari Arsenal wameondoka London na kutua salama jijini Munich, Ujerumani tayari kwa mchezo huo. Je, wauweza mzigo huo wa Kijerumani?

KAMA ULIFIKIRI SIMBA WAMEITANGULIZA YANGA, WANACHOWAZA NI KINGINE KABISAAAA... Wakati homa ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga ikizidi kupanda taratibu, Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ametamka kuwa hawana hofu hata kidogo na wapinzani wao hao huku wakiwaza mchezo wao unaofuata dhidi ya African Lyon. Vinara hao wa ligi watawavaa wapinzani wao wakuu Yanga kwenye mechi ya ligi itakayopigwa Februari 25, mwaka huu ambapo pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na tofauti ya pointi baina ya timu hizo. Mayanja amesema hawawezi kuwafikiria Yanga kutokana na mchezo wao kuwa mbali na kilichopo kwenye fikra zao ni kuangalia namna ya kulipa kisasi kwa Lyon kwenye mechi ya Kombe la FA (Shirikisho), Alhamisi ijayo. “Yanga hatuna wasiwasi nao kwa sababu mechi yao ipo mbali lakini hata ikija tutacheza kwa uwezo wetu kuhakikisha tunapata matokeo mbele yao na tunaamini tunaweza kufanya hivyo. “Lakini sasa tunaangalia namna ya kuwafunga Lyon kwenye mechi yetu inayofuata,” alisema Mayanja.

HIKI NDICHO ALICHOVUNJIKA JESUS WA MANCHESTER CITY Mshambuliaji Gabriel Jesus wa Manchester City amevunjika mfupa wa tano wa mguu maarufu kama metatarsal. Jesus ambaye alionekana ni mkombozi wa Man City katika ushambulizi alivunjika katika dakika ya 14 ya mchezo dhidi ya Bournemouth ambao City walishinda kwa mabao 2-0. Lakini tayari amepatiwa matibabu na na inaonekana maendeleo ni mazuri. TAKWIMU ZAKE PREMIER LEAGUE Mechi 4 Nafasi alizotengeneza 4 Mashuti yaliolenga 4 Mabao aliyofunga 3 Pasi za mabao 1

DI MARIA ATUPIA MBILI PSG IKIITULIZA BARCELONA KWA 'LAINI' YA 4G PSG imeonyesha inaweza baada ya kuitwanga Barcelona kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mbaingwa Ulaya. Barcelona ikiwa ugenini jijini Paris imeshindwa kuonyesha cheche licha ya kuongozwa na nyota wake Lionel Messi na Neymar na kujikuta ikipokea kipigo hicho cha kondoo mchovu. Angelo Di Maria ametumbukia nyavuni mara mbili huku Endson Cavani aliyetimiza miaka 30 jana akifunga moja na Julian Draxler akifunga moja. Mechi nyingine Benfica imeifunga Borussia Dortmund kwa bao 1-0.

YANGA WAPOKELEWA UWANJA WA NDEGE KWA MBWEMBWE ILE MBAYA Mashabiki wa Yanga wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuipokea timu yao ambayo imewasili leo ikitokea Comoro ambako iliitwanga Ngaya kwa mabao 5-1 katika mechi ya kwanza ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.