Jumatatu, 2 Januari 2017

Oscar ajaza mashabiki airport alivyowasili Shanghai China. Kutoka Chelsea ambapo alikua nyuma ya vivuli vya wachezaji wenzake kama wakina Diego Costa, sasa hivi amepata nafasi yake ndani ya China ambapo ameanza maisha mapya ya kuwa star. Midfielder Oscar ataungana na kocha wake wa zamani Adre Villas Boas ambaye anakiongoza kikosi cha Shangai SIPG. Oscar mwenye miaka 25 amekua gumzo baada ya kujaza mashabiki wengi kwenye uwanja wa ndege wakati anawasili huku wengi wao walikua wakitana sign kutoka kwa mchezaji huyo. Mchezaji huyu ambae analipwa £400,000 kwa wiki amesepa kutoka kwenye kikosi cha Chelsea kutokana na kutokua chaguo la kocha wa sasa Conte na kumfanya asicheze kabisa kwa muda mrefu. Hivi ndivyo Oscar alivyopokelewa na mashabiki wa Shanghai SIPG ya China.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni