pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 10 Januari 2017
Afcon 2017 inavyousogeza ubingwa Chelsea na kuziathiri timu nyingine. Ligi ya Uingereza iko katika hatua za lala salama ikiwa katika raundi ya pili.Chelsea wanaonekana kuzidi kulikaribia kombe wakiwa wameshinda mechi 13 mfululizo kabla ya kupoteza katika mchezo wake uliopita dhidi ya Totenham,hafi sasa EPL kumechezwa mechi 20 ambazo kimahesabu ni sawa na dakika 1800.Nakuletea jinsi mashindano ya mataifa ya Afrika Afcon yatakavyodhiathiri timu za Uingereza na kuzifaidisha timu nyingine haswa Chelsea kwenye mbio za ubingwa. Afcon inakuja kipindi ambacho baadhi ya timu zinahangaika kubaki kwenye ligi msumu ujao na nyingine zikitaka ubingwa bila kusahau ni kipindi ambacho FA inaendelea na EFL iko kwenye mtoano. Jose Mourinho alionekana kujawa na hasira baada ya Erick Bailly kuichezea Manchester kwa dakika 919 msimu huu kuondoka na kwenda kujiunga na timu yake ya taifa,si kwamba Mourinho hakujua kuhusu Bailly kuondoka kwenda nyumbani kujiunga na timu yake ya taifa lakini baada ya ushindi wa goli 2 dhidi ya Middlesbrough kocha Jose Mourinho aliamini atakuwa na Bailly katika mechi dhidi ya West Ham lakini haikuwa hivyo,Bailly alirudi nyumbani kitendo kilichomkera Mreno huyo kwani toka Bailly asajiliwe hajatumika vizuri Manchester kutokana na majeruhi na kipindi hiki ambacho yuko fiti anarudi nyumbani kuitumikia timu yake ya taifa na hivyo Manchester United kubakiwa na mabeki 3 wa kati ambao ni Phill Jones,Chris Smalling na Marcos Rojo. Huku Mourinho akikasirishwa na Bailly kurudi nchini kwao,mabingwa watetezi wa Leicester wamepoteza wachezaji wao tegemezi Ryad Mahrez ambae wiki hii pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na sasa anakwenda kuungana na mshambuliaji mwingine wa Leicester Islam Slimani huku Jeffrey Schullup na Daniel Amartey nao wakiondoka kwenda kuichezea Ghana na kumfanya Claudio Ranieri kuwa na wakati mgumu sana kupoteza wachezaji wake wanne kwa pamoja.Hii inawaapa wakati mgumu sana Leicester katika mbio za kutetea ubingwa wao haswa kutokana na matokeo mabovu msimu huu.Mahrez ameichezea Leicester kwa dakika 1511 msimu huu,Islam Slimani akicheza dakika 905 na Amartey akikipiga kwa dakika 1373 kati ya 1800 hadi sasa. Arsenal na Liverpool nao wapo katika mbio za ubingwa msimu huu lakini pia wanaathirika moja kwa moja na michuano ya Afcon,Sadio Mane amekuwa katika kiwango cha kuvutia na kumfanya awe kati ya wachezaji wanaopendwa sana na kocha Jurgen Klopp lakini baada ya mechi dhidi ya Sunderland alikwea pipa kurudi nyumbani kujiunga na timu yake ya taifa ya Senegal,Mane msimu huu ameichezea Liverpool kwa dakika 1659 vivyo hivyo kwa Arsenal wanaenda kumpoteza kiungo wao mkabaji Mohamed Elneny ambaye msimu huu amecheza dakika 533 anaeenda kuwatumia mafarao wa Misri. Southampton nao watakosa huduma ya Sofiane Boufal anaenda Morocco,Hull City ikiwapoteza Ahmed El Mohamedy anaeenda kuichezea Misri na Dieumerci Mbokami anyeenda Congo ambao jumla yao kwa pamoja waliichezea Hull kwa dakika 2318,Crystal Palace ambao wana kocha mpya Sam Allardayce wanaenda kumkosa Wilfred Zaha aliyeamua kurudi nyumbani Africa kulitumikia taifa lake la Ivory Coast huku winga huyo akiwa kaichezea Palce dakika1644 kati ya 1800 za msimu huu,Zaha anaondoka pia na Bakary Sako anayeenda Mali. Idrissa Gueye ni kati ya wachezaji waliocheza sana msimu huu Everton akiwa amecheza dakika 1669 lakini sasa anaenda kuungana na ,Stoke City nao watawapoteza Wilfred Bonny,Mame Ibram Diouf na Ramadhan Sobhi wanaorudi Africa,Diouf ameichezea Stoke dakika 893,Bonny 690 na Sobhi dakika 195,huko Sunderland Lamine Kone anaenda Senegal,Wahbi Khazri anaenda Tunisia,Kone amecheza dakika 1464 na Khazri akicheza dakika 452.Cheikhou Tiyote ataenda Senegal na Adre Ayew ataenda Ghana hukua Ayew akiwa amecheza dakika 500 na Kouyate akicheza dakika 1600 wameiacha West Ham na kurudi nyumbani. Wakati timu hizo zikiwakosa wachezaji hao kwa wakati huu ambao ligi kuu Uingereza iko raundi ya lala salama,na michuano ya EFL na FA kuendelea,Chelsea wataendelea kupata huduma ya wachezaji wao wote 11 kwani Muafrika pekee anayeanza katika timu hiyo Victor Moses timu yake ya Nigeria haipo kwenye michuano hii ya AFCON baada ya kushindwa kufudhu na kuzidi kuwapa nafasi ya kujivinjari kileleni mwa ligi,Totenham wataendelea kuwa na Wanyama kwa kuwa Kenya nao hawapo Afcon lakini Yaya Toure alijiuzulu kuitumikia timu ya taifa na hivyo ataendelea kuwepo katika kikosi cha Pep Guardiola na hii inaonekana kama faida kubwa kwa Conte na timu yake kuendelea kukaa kileleni mwa ligi. Ifuatayo ni orodha kamili ya dakika ambazo timu za Epl watazikosa wakati wa Afcon. Leicester 3793 Sunderland 3221 Hull 2328 Watford 2130 West Ham 2001 Stoke City 1778 Crystal Palace 1703 Everton 1669 Liverpool 1659 Manchester United 919 Southampton 625 Arsenal 533 Bournamouth 30 Chelsea 0 Man City 0 Totenham 0 Swansea 0 Burnley 0 Midllesbrough 0. West Brom 0.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni