Jumapili, 18 Desemba 2016

LIVE KUTOKA NANGWANDA SIJAONA: NDANDA FC 0-0 SIMBA (KIPINDI CHA PILI) Dakika ya 47: Timu zote bado zinasomana na mchezo umeanza kwa kasi ya taratibu. Kipindi cha pili kimeanza. MAPUMZIKO Dk 45+3, Ndanda wanaingia vizuri tena, kwoshi ya Kiggi, lakini Agyei tena anatokea na kudaka Dk 45+2 Ndanda wanaingia vizuri kabisa tena, wanapata kona, inachongwa na Kiggi, Agyei anapangua na mabeki Simba wanaondosha DK 45+1 Ndanda wanapoteza nafasi nzuri kabisa mabeki wa Simba wakiwa wamejisahau DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 45, Ajibu anapiga vizuri kabisa lakini ni goal kick DK 44, Simba inapata faulo baada ya Mo Ibrahim kuangushwa na Mtama. Si mbali. Dk 40, Simba wanapata nafasi nyingine, lakini Mo Ibrahim anashindwa kupiga shuti vizuri baada ya mpira kudunda kwenye uwanja Dk 36, Simba wanapata nafasi nyingine lakini Ajibu anachonga krosi fupi, Ndanda FC wanawahi Dk 35 sasa, Simba wanaonekana kuimarika katika nafasi ya kiungo. Hata hivyo bado hakuna mashambulizi makali huku ndanda wakionekana kupunguza mashambulizi tofauti na walivyoanza Dk 33, Simba wanapata kona nyingine, inachongwa vizuri, Blagnon anaruka na kupiga kichwa. Kipa anadaka kwa ulaini Dk 27, Ajibu anaingia na kupiga shuti kali, linamgonga beki wa Ndanda na kuwa konalakini haina faida Dk 24, Ndanda wanaingia vizuri tena, Mponda anapijga shuti kali lakini linaishia mikononi mwa Agyei Dk 22, Ndanda wanafanya shambulizi kali lakini Bokungu anatoa na kuwa kona. Inachongwa na Kiggi, haina faida Dk 18 sasa mpira bado hauna ladha sana na mashambulizi bado si makali SUB Dk 15 Yassin Muzamiru anaingia kuchukua nafasi ya Kotei ambaye anaonekana ameumia baada ya kugongwa kiwiko na Kiggi Dk 13, Mpira umesimama hapa baada ya kiungo wa Simba Kotei kugongwa kiwiko wakati akigombea mpira na Kiggi Makasi Dk 11, Agyei analazimika kufanya kazi ya ziada kupambana na mshambuliaji wa Ndanda ili kumpokonya mpira, tayari alishamtoka Mwanjale Dk 6, krosi nzuri ya Kigi Makasi lakini AAgyei anatoka na kudaka vizuri Dk 3, krosi safi ya Kichuya, inamfikia Blagnon anapiga kichwa lakini anashindwa kulenga lango Dk 2, Ndanda wanaingia tena hapa, Paul Ngalema anajaribu lakini Agyei anaudaka na kuanguka Dk 1, Ndanda wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Simba, anapiga shuti kali hapa Hamisi Rifat lakini hakulenga lango KIKOSI CHA SIMBA 1. Daniel Agyei 2. Bosaka Bukungu 3. Mohamed Zimbwe 4. Method Mwanjale 5. Abdi Banda 6. Jonas Mkude 7. Shiza Kichuya 8. James Kotei 9. Frederic Blagnon 10 Ibrahim Ajibu 11. Mohamed Ibrahim Benchi Peter Manyika Hamad Juma Said Ndemla Laudit Mavugo Jamal Mnyate Novaty Lufunga Mzamiru Yassin

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni