pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 2 Novemba 2016
LIVE KUTOKA SOKOINE MBEYA: MBEYA CITY 1 VS 0 YANGA
Dk 22, City wanagongeana vizuri tena, Mahundi hatari huyu, anaachia shuti kaliii, hatari kabisa unatoka sentimeta chache kabisa kwenye lando la Yanga
Dk 21, Yanga wanagongenaa vizuri hapa, mpira unamfikia Msuva anaachia fataki....wapiii
Dk 19, kipa wa Mbeya City anaokoa mpira hatari wa Donald Dombo Ngoma
SUB Dk 19 upande wa Mbeya City, Hemed Mlutabozwa anatoka baada ya kuumia, anaingia Hemed Ramadhani.
Dk 15, Mbeya City nao wanapata kona baada ya krosi ya Maundi kuokolewa na kutoka. Mwasapili ndiye anachonga hapaa, Yanga wanaokoa
Dk 14, Msuva anamtoka Mwasapili, krosi safi kabisa lakini City wanaokoa na kuwa kona ya pili
Dk 13, Msuva anaingia vizuri na kupiga krosi, inaokolewa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina matunda
Dk 11 sasa, bado Yanga wanaonekana hawajatulia wala kufanya shambulizi kali linaloweza kuwapa City presha
GOOOOOOO Dk 6, Hassan Mwasapili anapiga mpira unaojaa moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa Dida Munishi
Dk 1, kila timu imeanza taratibu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini hakuna inayocheza kwa papara.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni