Jumapili, 23 Oktoba 2016

Kwa mara ya kwanza Cristiano Ronaldo ameshindwa kufunga katika mechi 4 mfululizo kwenye uwanja Santiago Bernabeu (Michuano yote).

Cristiano Ronaldo alikosa nafasi nyingi za kufunga lakini Alvaro Morata aliyeingia kutoka benchi alikuwa shujaa baada ya kufunga goli la ushindi akiwa anaadhimisha birthday yake ya 24. Ronaldo ameonekana kukosa kujiamini katika mchezo huo licha ya kujaribu kufunga mara kadhaa. Takwimu zinaonesha alipiga mashuti 11 katika mchezo huo, mashuti meng zaidi ya mashuti yaliyopigwa na timu nzima ya Athletic Bilbao lakini ni mashuti mawili pekee ya Ronaldo yaliyolenga goli (on target). Nahodha huyo wa Ureno alikosa mechi za mwanzoni mwa msiku kutokana na kuwa majeruhi, amefunga magoli mawili tu kwenye mechi sita za La Liga alizocheza huku mechi zote Madrid ikiondoka na ushindi mnono. Alipata nafasi pekee baada ya Lucas Vazquez kumuwekea pande kwenye njia dakika za majeruhi wakati Athletic waliposhambulia golini kwa Madrid wakitafuta goli la kusawazisha. Real Madrid wamekwea kileleni mwa La Liga baada ya kupambana vikali kupata ushindi dhidi ya Athletic Bilbao. Karim Benzema aliipa Madrid bao la kuongoza kwa kuunganisha pasi ya Isco. Sabin Merino akasawazisha baada ya Pepe na Dani Carvajal kushindwa kuchukua mpira kwa Javier Eraso aliyepiga pasi ya mwisho. Madrid inaongoza La Liga ikiwa nafasi ya kwanza kwa ponti 21 baada kucheza mechi 9, Sevilla wanakamatia nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 20 wakati Barcelona wao wakiwa nafasi ya tatu na pointi zao 19 sawa na Villarrial lakini wanatofautiana watani wa kufunga na kufungwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni