pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Ijumaa, 2 Septemba 2016
ACACIA YATAJA SABABU ZA KUIPIGA CHINI STAND UNITED
Baada ya kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA kutangaza kusitisha udhamini kwa klabu ya Stand United ya Shinyanga, kampuni hiyo imeweka wazi sababu zilizowafanya kufikia uamuzi huo.
Afisa habari wa kampuni hiyo Necta Foya ametaja kuwa, mvutano wa viongozi katika klabu hiyo ndiyo sababu kubwa iliyopelekea wao kuachana na Stand United.
“Makataba wetu ulikuwa wa miaka miwili, kila baada ya mwaka mmoja tunafanya evaluation, kwahiyo wakati tunaevaluate kuna maeneo gani ambayo . kwahiyo kuna vitu ambavyo vilikuwa havijafanyika ndani ya makataba lakini vilevile kuna suala la changamoto ambazo zilikuwepo kwenye mambo ya uongozi”, Foya alikaririwa na Sports Extra ya Clouds FM.
“Kwahiyo kutokana na masuala mbalimbali, sisi ACACIA tukaona ni vizuri tuwaache hawa ndugu zetu wa Stand United kwasababu tumeshakaa nao na kuzungumza nao mara nyingi tu kwahiyo sio kitu ambacho tumekifanya ghafla”.
“Tumewasaidia ili waweze kujisogeza kwa miezi mitatu wakati wanajipanga upya, tumewapa dola za Marekani 60,000 kwa upande huo ni kwamba tumeweka wazi kabisa na kuna hela nyingine ambazo tulikuwa tunatakiwa kulipa kama dola 27,000 ikiwa ni malipo ya mishahara ya wachezaji”.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni