pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 28 Desemba 2016
Bingwa wa French Open 2008 mwanadada Ana Ivanovic apo jana ametangaza kustaafu kucheza tenesi akiwa na umri wa miaka 29. Mserbia huyo ambaye ni mke wa kiungo Bastian Schweisteiger, amekuwa akisumbuliwa na majeruhi na sasa anakamata namba 63 kwa ubora duniani baada ya kushinda michezo 16 tu katika mwaka 2016. . . Danke Ana 👋🏻🙏🏻
ULIISIKIA HII YA MAMBO KUMUENDEA POA IBRAHIM AJIBU KULE MISRI? Kiungo Ibrahim Ajibu sasa ana hadi nafasi ya asilimia 70 kupata nafasi ya kuitumikia Haras El Hodood ya Misri. Ajibu amepasi vipimo vya afya, maana yake nafasi ya kukipiga nchini Misri ni kubwa kama ambavyo taarifa zimeeleza. Amepewa muda wa wiki moja na nusu wa majaribio na unaisha Desemba 31. Abdel Haidar anayejishughulisha na masuala ya afya katika timu hiyo ya Jeshi la Misri, amezungumza na Championi kutoka Alexandria Misri na kusema hiyo ni hatua kubwa kwa Ajibu. “Amefuzu vipimo vya afya. Hii ni hatua kubwa zaidi, sasa yamebaki masuala baadhi ambayo yanamhusu kocha. “Kocha sasa anaendelea naye na mwisho atatoa maelezo kuhusiana na suala la vipimo vya afya,” alisema Haidar. Wakati Haidar anasema hivyo, Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji amesema wanasubiri kuhusiana na Ajibu hadi Desemaba 31. “Taarifa za maendeleo yake tunazifuatilia kwa karibu kabisa. Tunajua hilo la vipimo vya afya lakini sisi hatutalizungumzia kwa kuwa anaendelea na majaribio hadi Desemba 31. “Baada ya hapo, tunaamini timu hiyo itaanza mawasiliano nasi. Hivyo nafikiri mgevuta subira,” alisema Dewji maarufu mama Gwiji ambaye amewahi kuwa katibu mwenezi wa kikosi cha Simba kilichotinga fainali ya Caf mwaka 1993 na katibu mkuu wakati Simba ikiing’oa Zamalek Klabu Bingwa Afrika mwaka 2003. Kama Ajibu atakuwa amefuzu vipimo vya afya maana yake ni sawa na kufuzu kuichezea timu hiyo kwa asilimia 80. Hata hivyo, kama atafuzu na kujiunga nayo atakuwa na kazi ngumu kuhakikisha anapambana kuisaidia kurejea Ligi Kuu Misri baada ya kuwa imeshuka msimu uliopita. Kwa Tanzania, Haras El Hood kwa kile kipigo cha mabao 5-1 ilichokitoa kwa Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.
KOCHA ALIYENG'ARA TP MAZEMBE NI KATI YA WANAOWANIWA NA AZAM FC Pamoja na kwamba mambo yakiwa yameendelea kuwa siri kubwa, kuna taarifa kocha wa zamani wa TP Mazembe, Lamine N'Diaye, naye anaweza kutua Azam FC. N'Diaye raia wa Senegal ambaye aliwahi kukipiga katika kikosi cha Cannes ya Ufaransa, ni kati ya makocha wanaopewa nafasi ya kuinoa Azam FC. “Kweli kuna ishu ya Kali (Ongala). Anaweza kuanza kazi na timu halafu wakikubaliana na N'Diaye, basi anakuja kuwa bosi. “Unajua ni kocha mkubwa, Mazembe amekuwa hadi mkurugenzi wa ufundi. Ni mtu mtaalamu sana na soka la Afrika, usisahau aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Senegal,” kilieleza chanzo. N'Diaye aliisaidia Mazembe kuchukua makombe ya ubingwa wa Congo na makombe mengine, ubingwa wa Afrika kuanzia akiwa kocha na baadaye mkurugenzi wa ufundi. Azam FC imetangaza kumtimua Kocha Zeben Hernandez na makocha wasaidizi wote. N'Diaye alitua TP Mazembe mwaka 2010, baadaye mwaka 2013 akawa mkurugenzi wa ufundi. Lakini amewahi kufundisha timu ya taifa ya Senegal. Kabla aliifundisha Coton Sport ya Cameroon kwa mafanikio pia Maghreb Fez ya Morocco.
Kumbe Mourinho alipewa msaada na Fergie mambo yalivyomuendea kombo.Kwa muda kadhaa kabla ya Manchester united haijaanza kupata matokeo ya kushinda mechi ilikua inapoteza mechi nyingi sana tofauti na jinsi ilivyotegemewa. Taarifa zinasema kwamba Jose Mourihno ambae ana urafiki wa karibu sana na Sir Alex Fergie ambae kwa sasa ni board member wa Manchester united alikutana naye. Kukutana kwao inasemekana ilikua ni baada ya Manchester kuonekana inaenda kombo licha ya kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa. Katika mkutano wao huo wa siri licha ya kuongea mengi lakini inasemekana kitu kimoja wapo ambacho Fergie amemshauri Jose ni kuwa yeye kama zamani na kuacha ku-act up. Inasemekana Fergie alimwambia Mourinho awe kama kawaida alivyokua zamani. Vyombo vingine vya habari vimeandika kwambwa ni kama aibu kidogo kwa kocha mwenye uzoefu kama Jose kupata wakati mgumu hadi kuomba msaada. Lakini kwa Fergie atabaki kuwa na jukumu juu ya hilo kwasababu ndie board member pekee mwenye uzoefu wa uwanjani. Hivyo basi ana anafasi kubwa ya kumshauri vizuri kocha wao wa sasa. Baada ya ushindi dhidi ya Sunderland, Manchester wanategemewa kucheza dhidi ya Middlesbrough siku ya 31. Kwasasa Manchester united ipo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi, kazi yao kubwa ni kumaliza kwenye top 4 ili wapate nafasi ya kucheza UEFA Champions League msimu ujao.
Wachezaji 5 ambao Manchester wanaweza kuwaacha kwenye dirisha dogo. Tukikaribia muda wa dirisha dogo tunategemea kuona movement ya wachezaji wengi kwenda kwenye timu mbali mbali wakiziacha timu zao za sasa hivi. Tangu afike Manchester united Mourihno amekua akisajili wachezaji ana kujaza nafasi za wachezaji wengi kwenye namba kadhaa kufanya wachezaji hao wote wakubwa wakigombania namba moja. Pia hadi sasa bado kuna tetesi za kuleta wachezaji wapya ambao wanakuja kuongeza swala la kugombani namba. Hivi sasa Manchester united inategemewa kumkalibisha mchezaji Victor Lindelog kutkka Benfica. Hawa ni wachezaji watano ambao huenda wasivae tena jezi ya Manchester united baada ya muda dirisha dogo kufika. Memphis Depay. Bila shaka huyu jamaa mwenye miaka 22 amepitia wakati mgumu kuonyesha uwezo wake ndani ya Old trafford tangu ahamie kutoka PSV. Depay amecheza dakika 22 tu tangu msimu huu wa uanze kwenye ligi. Hivi sasa anategemewa kujiunga na club ya Everton kwa mkopo ili akapate muda zaidi wa kucheza. Marouane Fellaini Fellaini hajawai kuwa kipenzi cha Old Trafford na umaarufu wake unatokana na mabaya ya kusababisha magoli zaidi ya kusababisha magoli ili timu yake ishinde. Aliwai kuzomewa na mashabiki lakini bado kocha Jose anaendelea kumpa namba japo kwa dakika chake. Sasa hivi ameamua kwenda zake Milan ambapo ameshaonekana maeneo hayo siku chache zilizopita. Bastian Schweinsteiger Huyu jamaa alitegemea maisha mazuri ndani ya Manchester united chini ya Van Gaal. Lakini baada ya kuja kocha mpya amekosa kabisa imani naye na bila shaka anatakiwa kutafuta njia nyingine. Anategemewa kwenda kwenye ligi ya marekani. Morgan Scheiderlin Alivyotoka Southampton vitu vingi vilitegemewa lakini haukua hivyo. Imekua ni disappointment kubwa kwa central midfielder huyu. Anategmewa kwenda pamoja na Depay kwenye club ya Everton. Anthony Martial Kuna asilimia chache sana kama mchezaji huyu anaweza kusepa Manchester united. Tofauti na wenzake, Martial ameonekana akifanya juhudi na kufunga magoli. Hivyo basi hakuna uhakika kama anaweza kusepa kwenye club hii au la.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)