Jumatano, 4 Januari 2017

FT Spurs 2- 0 Chelsea Dele Alli 45' 54'

AZAM FC YAAMBULIA SULUHU KWA JAMHURI, BOCCO AIZUNGUMZIA YANGA, ASEMA KAZI IPO Azam FC inalazimika kuisunga Yanga ili kufuzu katika hatua ya mtoano ya Kombe la Mpinduzi. Hiyo inatokana na matokeo ya mchezo wao wa leo baada ya kupata sare ya bila mabao dhidi ya Jamhuri kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo usiku. Hata hivyo, John Bocco ambaye ni nahodha wa Azam FC, amesema kazi ni ngumu kwa kuwa Yanga ni timu kubwa. “Tunawaheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa. Tunajua nasi ni timu kubwa na bora, itakuwa mechi ngumu sana. “Lakini tunaiweka kando mechi ya leo na tunaanza maandalizi kwa ajili ya mechi ijayo kujiandaa dhidi ya Yanga,” alisema. Kabla ya kukutana na Azam FC leo, Jamhuri ilikuwa imekutana na dhoruba ya kipigo cha mabao sita kutoka kwa Yanga.

Msuva anaendelea kuwatesa magolikipa wa Mapinduzi Cup 2017 Simon Msuva ameendelea kuwa bora uwanjani na kuisaidia timu yake kupata ushindi kwenye michuano ya Mapinduzi Cup baada ya kutupia bao mbili kambani na kuifanya Yanga kufikisha pointi 6 na kukaa juu ya Kundi B. Kama angepata mkwaju wa penati angekuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwenye mashindano ya msimu huu na kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuibuka mfungaji bora wa michuano ya Mapinduzi 2017. Msuva alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 11 kwa kuiwahi pasi ndefu iliyopigwa na kiungo Thaban Kamusoko, bao lake la pili amelifunga dakika ya 21 bao ambalo limemfanya afikishe magoli manne katika mashindano ya mwaka huu kufuatia kufunga magoli mawili kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Jamhuri wakati Yanga ilipoifunga Jamhuri magoli 6-0. Hadi sasa Msuva ndiye anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa na magoli manne akifatiwa kwa karibu na Labama mwenye magoli matatu. January 7 Yanga itacheza na Azam FC mchezo wa tatu katika hatua ya makundi mechi inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi wote wa soka kutokana na upinzani uliopo kati ya vilabu hivi viwili.

Spurs VS Chelsea…Thierry Henry ataja upande wake..Arsenal wewe utakua wapi? Ukiangalia Chelsea kwa jinsi inavyoenda kwa kasi basi leo inabidi mashabiki wa Arsenal kuwaipe support Spurs. Lakini kwa baadhi ya mashabiki wa Arsenal wataleta ugumu wa kukata kui support Spurs kutokana na ushindani uliopo kati yao. Kinachotakiwa leo ni Spurs kushinda ili iwapunguze kasi Chelsea kwenye njia yao kuelekea ubingwa. Kama wakifungwa watarudishwa point tatu nyuma badala ya kwenda mbele. Sasa kwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry amesema kwake yeye ni ngumu sana kuwa upande wa Spurs. Henry aliulizwa na mtangazaji kuhusu upande wake kama atakuwa kwa Spurs, “Sitakua huko, labda watu wengine au wao watakua kwetu lakini sio mimi. Hiyo itakua ngumu sana kwangu”. Je, wewe ni shabiki wa Arsenal?, utakua upande gani usiku wa leo?.