Jumanne, 3 Januari 2017

CHELSEA HAWA HAPA KABLA YA MECHI YAO YA KWANZA MWAKA 2017 LEO Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea leo wanashuka dimbani kuwavaa Tottenham Hotspurs. Itakuwa ni mechi yao ya kwanza mwaka 2017. Vinara hao wana mechi ngumu kweli mbele yao lakini wamefanya maandalizi ya kutosha na wako tayari. MATOKEO YAO October 1: Hull 0-2 CHELSEA October 15: CHELSEA 3-0 Leicester October 23: CHELSEA 4-0 Manchester United October 30: Southampton 0-2 CHELSEA November 5: CHELSEA 5-0 Everton November 20: Middlesbrough 0-1 CHELSEA November 26: CHELSEA 2-1 Tottenham December 3: Manchester City 1-3 CHELSEA December 11: CHELSEA 1-0 West Brom December 14: Sunderland 0-1 CHELSEA December 17: Crystal Palace 0-1 CHELSEA December 26: CHELSEA 3-0 Bournemouth December 31: CHELSEA 4-2 Stoke

Ushindi wa Simba vs KVZ ulivyobeba maana ya January 3 kwa Mzamiru Kama ulikua hujui, jana January 3 ilikuwa ni birthday ya Muzamiru Yassin kiungo anayefanya vizuri kwa sasa kwenye klabu ya Simba na ligi kuu Tanzania bara kutokana na kiwango kizuri anachokionesha uwanjani. Wakati anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Simba ilikuwa ina ratiba ya kucheza mechi ya mapinduzi Cup dhidi ya KVZ. Mzamiru amesema siku ya leo muda mwingi alikuwa akiomba kwa Mungu aisaidie timu yake kupata ushindi na imetokea hivyo huku goli la ushindi akifunga yeye mwenyewe. Mzamiru amesema hatoisahau birthday yake ya mwaka huu kwa sababu amefanikiwa kufunga goli lililoipa Simba ushindi muhimu kwenye michuano ya Mapinduzi. “Nilikua namuomba sana Mwenyezi Mungu siku yangu ya kuzaliwa niipatie timu yangu ushindi na nashukuru imetokea kama nilivyooma,” anasema Mzamiru ambaye alisajiliwa na Simba kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro. Kama kawaida, birthday za siku hizi kuogeshwa ni imekuwa ni desturi. Wachezaji wa wenzake wa Simba walimuogesha kama ku-show love kwa mshkaji wao. “Nimeongeshwa sana matope, juice bila kusahau maji.” Jambo la kuvutia ni kwamba, Mzamiru ndiye aliyefunga goli pekee la Simba lililoipa ushindi wa goli 1-0. “Birthday zangu huwa siziandai kwa sababu mara nyingi huwa nakuwa kwenye mashindanio, mwaka jana pia nilikuwa kwenye mashindano haya (Mapinduzi Cup) wakati bado nipo Mtibwa. Lakini hii nitraikumbuka sana kwa sababu nimeisaidia timu yangu kupata ushndi na kama tungepoteza mechi hii ningesikitika sana.” “Sasa hivi napata nafasi ya kufunga kwa sababu nacheza nyuma ya mshambuliaji mmoja.”

PICHA3: Ibrahim Ajib ndani ya uwanja wa Amaan, Zanzibar Mshambuliaji wa klabu ya Simba Ibrahim Ajib yupo ameungana na timu yake baada ya kurejea kutoka Misri alikukokuwa akifanya majaribio kwenye kloabu ya Haras Al Hodoud. Ajib ameonekana kwenye uwanja wa Amaan wakati Simba ikicheza mechi ya Mapinduzi Cup dhidi ya KVZ. Hadi sasa bado hakuna taarifa rasmi kutoka uongozi wa Simba wala Al Hodoudkama Ajib amefanikiwa katika majaribio yake au vinginevyo.

Mpya kuhusu Farid Musa na timu yake ya Hispania Kiungo mshambuliaji wa Tanzania Farid Musa amepost ujumbe kwenye account yake ya Insagram (farid_mussa17) akieleza hali ilivyo baada ya kuwasili kwenye klabu yake mpya ya Tenerife ya Hispania. Farid aliondoka Bongo usiku wa December 28 kuanza safari ya kuelekea Hispania kujiunga na Tenerife baada ya kusubiri kwa muda mrefu kibali cha kufanya kazi nchini huko ambacho mchakato wake ulichukua muda mrefu hadi kukamilika. “Thanks God nimeanza mazoezi leo na timu yangu mpya wameshanifanyia medical test ninachosubiri sasa ni leseni kutoka chama chao cha mpira cha Spain.” “Nimeanza maoezi na timu ya U-23 kwa sababu wanajaribu kunifundisha mfumo wanaoutumia kucheza mechi mbalimbali za U-23 huku nikisubiri leseni yangu, kikubwa kwangu namuomba Mungu aendelee kunipa moyo wa subra nina imani kila kitu kitakuwa sawa.” Mompondazy inaungana na wapenda soka wote kumtakia kila laheri Farid Musa katika timu yake mpya huko Hispania.

Ushindi mwingine umeiongezea Simba pointi Mapinduzi Cup 2017 Simba imefikisha pointi 6 baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 mbele ya KVZ kwenye mchezo wao wa pili wa Kundi A michuano ya Mapinduzi Cup 2017. Bao pekee la ushindi wa Simba limefungwa na kiungo Mzamiru Yassin dakika ya 44 kipindi cha kwanza ambalo lilidumu kwa muda wote uliosalia. Simba wamepata ushindi wa pili mfululizo baada ya kushinda 2-1 kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Taifa Jang’ombe wakati KVZ wao wamepoteza mechi zao mbili na kujiweka kwenye nafasi finyu ya kusonga mbele. Ratiba ya leo Jumatano January 4, 2017 Kundi B Saa 10:00 jioni Yanga vs Zimamoto Saa 2:15 usiku Jamhuri vs Azam

Antoine Griezmann amaliza story za kuelekea Manchester United.

Jang’ombe Boys imepata ushindi kwa mabigwa watetezi Mapinduzi Cup Jang’ombe Boys imekuwa timu ya pili kutoka Zanzibar kupata ushindi kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2017. Boys wameifunga URA FC ya Uganda kwa magoli 2-1 na kuchukua pointi tatu muhimu ikiwa ni mechi ya pili kwa timu hizo zilizopangwa Kundi A. Magoli ya Jang’ombe Boys yamefungwa na Khamis Mussa ‘Rais’ dakika ya 16 na 31 wakati Labama Bogota akifunga bao pekee la URA huku likiwa ni bao lake la tatu kwenye mashindano. Awali Taifa Jang’ombe ndio ilikuwa timu pekee ya Zanzibar iliyopata ushindi kwa kuifunga Jang’ombe Boys kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano hii uliochezwa December 30. January 1 KVZ ambayo ni timu nyingine ya Zanzibar ilipoteza mchezo wake mbele ya URA kwa magoli 2-0. Azam FC wakaifunga 1-0 Zimamoto huku Yanga ikiishushia gharika Jamhuri kwa kipigo cha 6-0 na kuzifanya timu za Zanzibar zikishindwa kufurukuta kwa wageni wao.