pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 2 Januari 2017
LWANDAMINA APANGA FULLU MZIKI YANGA IKIIVAA JAMHURI MAPINDUZI CUP LEO KIKOSI CHA YANGA SC DHIDI YA JAMHURI LEO (Mechi inatarajia kuanza Saa 2:30 usiku kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.) KIKOSI 1. Deogratius Munishi 2 Juma Abdul 3. Mwinyi Haji 4. Kelvin Yondani 5. Vicent Andrew 6. Justin Zulu 7. Saimoni Msuva 8. Thabani Kamusoko 9. Amissi Tambwe 10. Haruna Niyonzima 11. Emanuel Martin Akiba - Ali Mustafa - Hassan Hamisi - Nadir Haroub - Juma Mahadhi - Deusi Kaseke - Obrey Chirwa
BAADA YA DAKIKA 270 BILA YA KUFUNGA, KICHUYA HUYU HAPA ANAELEZA ANACHOKIONA Kiungo mwenye kasi wa Simba, Shiza Kichuya ameweka bayana kuwa kutofunga bao katika mechi tatu mfululizo ambazo ni sawa na dakika 270 kunasababishwa na ushindani uliopo kwa wapinzani wao ambao wengi wao wanacheza kwa tahadhari na kujilinda sana lakini anafurahia kuona wenzake wanafunga huku yeye akihusika kwenye mabao hayo. Kichuya ndiye kinara kwenye chati ya ufungaji akiwa sawa na washambuliaji wa Yanga, Simon Msuva na Amissi Tambwe ambapo kwa pamoja wana mabao tisa waliyoyafunga kwenye mechi 18 za ligi mpaka sasa. Winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema kuwa, hali ya ‘ubutu’ iliyomkuta imechangiwa na mabadiliko makubwa ya timu kwenye kipindi hiki cha mzunguko wa mwisho ambapo kila mmoja anajitahidi kucheza kwa umakini kwa ajili ya kuhakikisha hawafungwi. “Siyo kama sifungi kwa sababu kiwango kimeshuka, hapana ila tu sasa hali ya ushindani imebadilika kwa sababu kila timu inakomaa kuona haifungwi na hata kama ikipoteza basi siyo kwa mabao mengi, jambo hilo ndiyo limechangia mpaka sasa kwenye mechi tatu sijafunga bao lolote. “Lakini hata hivyo bado nina furaha kwa sababu timu inapata ushindi na wenzangu wanafunga na tunaendeleza kupata pointi tatu ambazo ndiyo lengo letu kwenye kila mechi na suala la kufunga siyo muhimu sana japo itakapotokea nafasi nitafanya hivyo,” alisema Kichuya.
MTANDAONI, AJIBU NI MALI YA HARAS EL HODOOD, HAJI MARA AFAFANUA KUHUSIANA NA USAJILI HUO Haras El Hodood ya Misri imetupia mtandaoni na kueleza kuwa mshambuliaji Ibrahim Ajibu ni mchezaji wao mpya. Ajibu anaonekana akiwa kwenye picha na wachezaji wengine wa Haras El Hodood ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Misri. Hata hivyo, Msemaji wa Simba, Haji Manara amelifafanua jambo hilo kwa kusema Ajibu bado ni mali ya Simba. “Nimeliona hilo suala, naulizwa sana. Lakini ukweli Ajibu bado ni mali ya Simba, bado hatujakaa mezani na hao ndugu zetu kuhusiana naye,” alifafanua. Simba ilitoa ruhusa ya Ajibu kwenda kufanya majaribio hadi Desemba 31, 2016 na baada ya hapo kama amefuzu, pande hizo mbili zingekaa mezani. Lakini tayar Haras El Hodood ilitangaza kwamba Ajibu alifuzu vipimo vya afya. Hivyo lilibaki suala la benchi la ufundi kuamua
Jumapili, 1 Januari 2017
SIMBA YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI, LUIZIO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR SIMBA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Taifa Jang’ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Hadi mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Muzamil Yassin na Juma Luizio. Kiungo Muzamil Yassin alianza kuifungia Simba dakika ya 27 baada ya kuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi kufuatia shuti la beki Mzimbabwe, Method Mwanjali ambalo lilimshinda kipa Ahmed Suleiman. Mshambuliaji Juma Luizio akafunga kwa shuti la umbali wa mita 17 baada ya kuwatoka mabeki wawili wa Taifa, kufuatia pasi ya Muzamil Yassin. Luizio anayecheza kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia akiichezea kwa mara ya pili Simba leo, alidumu uwanjani kwa dakika 60 tu kabla ya kumpisha Mrundi, Laudit Mavugo. Beki wa kati wa Simba, Novaty Lufunga akajifunga kwa kichwa katika harakati za kuokoa mpira wa kona uliochongwa na Hassan Bakari dakika ya 76 kuipatia Taifa bao la kufutia machozi. Katika mchezo uliotangulia, URA iliichapa 2-0 KVZ. Simba sasa inalingana kwa pointi na URA na Taifa iliyoifunga Jang’ombe Boys 1-0 katika mchezo wa kwanza Ijumaa. Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Daniel Agyei, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya/Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin, Juma Luizio/Laudit Mavgugo dk60, Said Ndemla na Jamal Mnyate/Moses Kitundu dk66. Taifa Jang’ombe; Ahmed Suleiman, Adam Hamad, Saleh Mgeni/Hassan Bakari dk59, Abdallah Shaibu, Samir Yahya, Khatib Simai, Ally Mlanga, Baraka Ushindi/Mohmed Salum ‘Messi’ dk56, Seif Hassan, Adam Ibrahim/Method Apigi dk62 na Yahya Tumbo/Nelson Gabriel dk72.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)