Alhamisi, 1 Desemba 2016

AZAM FC KUSAKA VIJANA U-17 KIGOMA J’MOSI HII KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, itakuwa mkoani Kigoma wikiendi hii Jumamosi (Desemba 3, 2016) kusaka vipaji vya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17). @ Azam FC will be in Kigoma this weekend as we host the penultimate trial for players under the age of seventeen (U17). The open trial will take place at the Lake Tanganyika Stadium this Saturday (3rd December) from 0800-1400. The trial will be open for players born from 2004-2000. #AzamFCU17Project

Wawa kafanya kweli kwa mzazi mwenzake BEKI wa zamani wa Azam FC, Serge Pascal Wawa amefunga ndoa na mzazi mwenzake aliyezaa nae watoto watatu. Wawa amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram picha zinazomuonyesha akiwa na mwanamke huyo katika nyuso za furaha huku akipokea salamu za pongezi toka kwa marafiki kutoka sehemu mbalimbali duniani. Wawa amerejea kwenye timu yake ya zamani ya El-Merreikh ya Sudan baada ya kumaliza mkataba wake na matajiri wa Ligi Kuu ya Vodacom na hakutaka kuongeza mkataba kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokuwa na uhusiano mzuri na Kocha Mhispania, Zeben Hernandez.

ZULU AWAAMBIA YANGA WAMPE MUDA KIDOGO, WATAFURAHI WENYEWE Kiungo mkabaji, Justice Zulu raia wa Zambia ambaye ametua nchini kumalizana na Yanga, amesema atakuwa fiti baada ya siku chache na wao Yanga watafurahi. Zulu anajiunga na Yanga baada ya kuwa amekaa nje kwa kipindi cha zaidi ya miezi minne bila ya kucheza baada ya kukumbana na adhabu ya Fifa, akituhumiwa ‘kumzika’ wakala wake. “Amesema atakuwa fiti hasa baada ya muda mfupi ingawa alishaanza mazoezi ya kujifua mwenyewe kabla ya kuja nchini,” kilieleza chanzo. Ujio wa kiungo huyo, unaonekana wazi kuwa unahitimisha kuwepo kwa Mbuyu Twite, beki kiraka wa Yanga ingawa kuna mjadala mambo yanaweza kubadilika na Zulu akachukua nafasi ya Vicent Bossou.

Kipa kafunga goli kwa Tik Tak dakika ya 95 Kipa huyu ameingia kwenye vichwa vya habari huko England toka South Africa ambapo ameikoa club yake kupoteza point zote kwenye mechi ya ligi kuu ya South Africa. Kipa Oscarine Masuluke wa Baroka FC alipiga tik tak kwenye kona ya gombani goli dhidi ya Orlando Pirates na kufanya matokeo yaishe 1-1. Wakati timu ikiendelea ku struggle dakika ya 95 zikiwa zimebaki sekunde game kuisha, ikapigwa kona na kipa akaenda kushambulia pamoja na wachezaji wenzake. Mpira kati kipa wa Orlando kapangia, ukaingia kati kipa wa Baroka FC akapiga tik tak hatari mpira nyavuni. Kila timu ikamaliza na poinrt zake moja moja.

DONE DEAL: Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji Kiungo mkabaji raia wa Zambia Justine Zulu amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga mabingwa watetezi wa taji la VPL na Azam Sports Federation Cup (FA Cup). Zulu alikua akiichezea Zesco United ya Zambia ambayo ilikuwa chini ya kocha wa sasa wa Yanga George Lwandamina ana miaka 27 huku akiwa na uzoefu unaotokana na kucheza soka la kulipwa nje ya Afrika pamoja na Afrika kwenye ligi zenye ushindani ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini. Zulu amewahi kuvitumikaia vilabu vya National Assembly, Hapoel Be’er Sheva, Hapoel Bnei Lod, Hapoel Rishon LeZion, Enosis Neon Paralimni, Lamontville Golden Arrows, Kabwe Warriors na ZESCO United. Mwaka 2012 alisaini miaka mitatu kuitumikia klabu ya Lamontville Golden Arrows ya Afrika Kusini. October 2013 alirejea kwenye ligi ya Zambia na kujiunga na Kabwe Warriors, ukiwa ni mkataba wa muda mfupi. Baadae alijiunga na Zesco United kuelekea msimu wa 2014 ambapo ameendelea kuhudumu hadi sasa. Mwaka 2011 alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Zambia. Zulu alikuwa sehemu ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2012 lakini hakufanikiwa kutajwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 waliotwaa taji hilo mwaka 2012. Wasifu wa Justine Zulu Date of birth11 August 1989 (age 27) Place of birthLusaka, Zambia Height1.82 m (5 ft 11 1⁄2 in) Playing positionMidfielder Club information Current teamZESCO United Senior career* YearsTeamApps(Gls) 2005–2007National Assembly 2007–2009Hapoel Be’er Sheva23(1) 2009–2010 Hapoel Bnei Lod 31 (1) 2010–2012 Hapoel Rishon LeZion 50 (3) 2012 Enosis Neon Paralimni 11 (0) 2012–2013 Lamontville Golden Arrows 4 (0) 2013 Kabwe Warriors 2014– ZESCO United

Hawa mashabiki wa Arsenal washangaza watu ndani ya Emirates Stadium. Picha kadhaa zilizopigwa kwenye mechi tofauti za Arsenal kwenye uwanja wa Emirates zimeshangaza watu na kaunza ku trend kwenye mitandao. Kwa kawaida inajulikana kwamba shabiki akienda uwanjani lazima anafuata kuangalia mechi ya timu yake. Lakini hawa wawili wamekua tofauti sana. Picha ya kwanza inamuonyesha jamaa mmoja asiyejulikana jina lake akitumia muda karibia wa kipindi kizima cha kwanza aki-fanya video call na mwanamke ambae inawezekana akawa ni mpenzi wake. Inakuaje kipindi kizima cha kwanza shabiki aliyelipia pesa nyingi kuingia kwenye Emirates stadium anaaaa kuongea na simu wakati wenzake wapo busy na kuangalia soka. Shabiki wa pili alionekana kuwa ni teenager ambae yupo busy anafanya homework yake ndani ya uwanja wakati mechi inaendelea. Hiki kitendo ni cha kawaida wanafunzi wakiwa wanaangalia mechi kwenye Tv lakini sio uwanjani. Inaonekana hakuna sababu ya kulipia ticket na kuingia uwanjani na madaftari yako ukafanye home work.

Zidane amzungumzia mwanae Enzo kwenye mechi ya kwanza na goli Ni mara chache sana huwa inatokea baba anakua kocha wa mwanae kwenye timu kubwa kama Real Madrid. Hivyo ndivyo inavyotokea sasa hivi kwa Zidane na Enzo.  Enzo mwenye miaka 21 alicheza club ya vijana ya Juventus kabla hajahamia Real Madrid ambapo alikua chini ya baba yake. baada ya Zidane kupewa majuku ya kikosi cha kwanza amemjaribu kwa mara ya kwanza mwanae kwenye mechi ya Copa del Rey jana.  Enzo ameingia mara ya kwanza na amefunga goli, “Nina jivunia kwa Enzo kama kocha na kama baba yake. Najivunia kikosi kizima jinsi walivyocheza leo usiku. Tumepata tulichokitaka huku tukiwapa nafasi vijana wadogo kucheza kwenye mechi ya jana.”  Enzo anavaa jezi yenye jina la Enzo badala ya Zidane ilikuepusha kufananishwa na makali ya baba yake uwanjani.