Ijumaa, 10 Machi 2017

AZAM FC WAWAOMBA SIMBA WAKAWASHANGILIE YANGA UWANJA WA TAIFA Uongozi wa Azam FC umewaambia wapenzi na mashabiki wa Simba na timu nyingine, waungane kwa pamoja kuishabikia Yanga, kesho Jumamosi itakapocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd huku akisisitiza kwamba kufanya hivyo ni uzalendo ambao unatakiwa kuanzia sasa na kuendelea. Yanga itacheza dhidi ya Zanaco katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mshindi atacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo. Upande mwingine, Azam FC yenyewe itacheza dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, keshokutwa Jumapili. “Kwa sasa lazima tukubali tu kwamba Yanga na Azam ndiyo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, hivyo litakuwa jambo la busara kwa mashabiki wote kuweka itikadi zetu pembeni na kuuungana pamoja kuhakikisha timu hizi zinafika mbali. “Nawaomba tu mashabiki wote, wa Azam, Simba na timu nyingine Jumamosi tukaishangilie Yanga pale Taifa, kisha Jumapili, tuungane tena kwenda Azam Complex kuishangilia Azam,” alisema Idd.

MAOFISA WA TFF WASHINDA SAKATA LA RUSHWA MAHAKAMA YA KISUTU Maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wameshinda kesi yao ya tuhuma za rushwa. Juma Matandika ambaye ni Msaidizi wa Rais wa TFF Jamal Malinzi, na Martin Chacha aliyekuwa mkurugenzi wao mashindano wa TFF. walikua wananashtumiwa kuomba rushwa ya milioni 25 kwa viongozi wa timu ya Geita Gold Sports ameachiwa huru Leo Sauti ziliolewa kuwa ni zao, zilisikika zikieleza mipango ya kuisaidia Geita Gold Sports na ilitakiwa fedha kwa ajili pia ya kuwapa viongozi wengine. Ingawa wadau wengi wanaojua sauti zao waliamini ni wao kabisa, lakini Mahakama ya Mkazi Kisutu imetupilia mbali ushahidi wa sauti uliowasilishwa mahakamani hapo.