Spurs VS Chelsea…Thierry Henry ataja upande wake..Arsenal wewe utakua wapi? Ukiangalia Chelsea kwa jinsi inavyoenda kwa kasi basi leo inabidi mashabiki wa Arsenal kuwaipe support Spurs. Lakini kwa baadhi ya mashabiki wa Arsenal wataleta ugumu wa kukata kui support Spurs kutokana na ushindani uliopo kati yao.
Kinachotakiwa leo ni Spurs kushinda ili iwapunguze kasi Chelsea kwenye njia yao kuelekea ubingwa. Kama wakifungwa watarudishwa point tatu nyuma badala ya kwenda mbele.
Sasa kwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry amesema kwake yeye ni ngumu sana kuwa upande wa Spurs. Henry aliulizwa na mtangazaji kuhusu upande wake kama atakuwa kwa Spurs, “Sitakua huko, labda watu wengine au wao watakua kwetu lakini sio mimi. Hiyo itakua ngumu sana kwangu”.
Je, wewe ni shabiki wa Arsenal?, utakua upande gani usiku wa leo?.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni